MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaagiza viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Padri Dk. Charles Kitima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Chalamila amesema kuwa kauli za kiongozi huyo wa kidini kuwa Tanesco walikata umeme siku aliyovamiwa na watu wasiojulikana waliomjeruhi.
Agizo hilo amelitoa leo alipokuwa akizungumza na wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ambapo amesema kauli za Dk. Kitima zinalichafua shirika hilo la Taifa.
“Nimewaambia jambo hili ni kubwa sana na limetolewa na kiongozi wa kidini, yaani hili shirika la Taifa linashirikiana na wahalifu ili auwawe?
“Twende mbele zaidi kwa Tanesco kuchukua hatua za kisheria, pia muangalie humo ndani inawezekana kuna watu wenu wameshiriki. Sasa mkienda huko ndiko tutajua ukweli,” amesema.
Amesema taifa hivi sasa linahitaji uponyaji na si viongozi wa dini kuchochea chuki na migawanyiko.
“Kiongozi anapogeuka mwanaharakati na kutoa kauli za mihemko ni hatari kwa jamii. Ni vema wakachunga kauli zao na wasijielekeze kusiko,” amesema.
ZINAZOFANANA
Uwezekano wa wanawake kuwa Mashemasi bado mgumu
Shule za sekondari, Veta kufungiwa miundombinu ya nishati safi ya kupikia
Meta yamjibu Mange Kimambi, yeye akimbilia kwa Trump