December 4, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wanafunzi 937,581 wachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wasichana vinara

Profesa Riziki Shemdoe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI)

 

SERIKALI imetangaza jumla ya wanafunzi 937,581 wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika muhala wa masomo wa Januari mwaka 2026 huku idadi ya wasichana wakiwa vinara wakiongozwa kwa wingi wanafunzi waliopenya kwenye zoezi hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa idadi ni wasichana 508,477 huku wavulana 429,104 hivyo wasichana wakiongozwa wavulana kwa idadi tofauti ya wasichana 79373 watakaojiunga na elimu ya upili (sekondari kwa mwaka 2026).

Tangazo hilo limetolewa leo tarehe 4 Desemba 2025 na Profesa Riziki Shemdoe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Prof. Shemdoe amesema kuwa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka wa masomo, 2026 umezingatia kigezo cha ufaulu wa mtahiniwa anayechaguliwa. shule za sekondari za bweni za serikali zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni shule za sekondari za bweni za wanafunzi wenye ufaulu wa juu (Special Schools), shule za sekondari za bweni za amali na Shule za Sekondari za bweni ni za Kitaifa hivyo, zimepangiwa wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuzingatia mgawanyo wa nafasi uliobainishwa na vigezo vilivyowekwa ili kuimarisha utaifa.

Uchaguzi wa wanafunzi katika makundi hayo ulifanyika kwa mujibu wa mwongozo wa uchaguzi wa mwaka 2024 kama ifuatavyo shule za sekondari za bweni kwa wanafunzi wenye ufaulu wa juu nafasi katika shule za wanafunzi wenye ufaulu wa juu zimegawanywa kwa kila mkoa kulingana na idadi ya watahiniwa wa darasa la saba waliotahiniwa katika mkoa husika kwa kutumia kanuni ya kugawa nafasi hizo kitaifa.

Jumla ya wanafunzi 937,581 wakiwemo wasichana 508,477 na wavulana 429,104 ikijumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalum 3,228 wakiwemo wasichana 1,544 na wavulana 1,684 wamepangwa katika shule za sekondari za Serikali 5,230 kwa ajili ya kuanza masomo ya Kidato cha kwanza mwaka, 2026 kwa mgawanyo ufuatao:-

“Jumla ya wanafunzi 815 wakiwemo wasichana 335 na wavulana 480 wamechaguliwa kujiunga katika shule za sekondari ambazo hupokea wanafunzi wenye ufaulu wa alama za juu. Shule hizo ni pia, amesema jumla ya wanafunzi 3,441 wakiwemo wasichana 1,279 na wavulana 2,162 wamechaguliwa kujiunga na shule za amali bweni.

Aidha,jumla ya wanafunzi 7,360 wakiwemo wasichana 5,014 na wavulana 2,346 wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni za Kitaifa “jumla ya wanafunzi 925,965 wakiwemo wasichana 501,849 na wavulana 424,116 wamechaguliwa kujiunga katika shule za sekondari za Kutwa ambazo hupokea wanafunzi kutoka katika eneo la karibu na shule ya msingi aliyosoma mwanafunzi husika

Prof. Shemdoe amesema,Serikali ilifanya maandalizi mapema ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote watakaofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka, 2025 wanajiunga na Elimu ya Sekondari ifikapo Januari, 2026.

Vilevile, nawashukuru viongozi wa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Halmashauri, wakuu wa shule, walimu na wadau wa elimu nchini kwa kutoa ushirikiano katika kusimamia uendeshaji na utoaji wa elimu ya msingi na sekondari nchini.

About The Author

error: Content is protected !!