December 4, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Ujumbe umefika, watawala wamepotezea

Rais Samia Suluhu Hassan

 

UJUMBE wa kudai haki umewafikia watawala na kwa namna nyingine wameamua kusema kuwa haki haidaiwi kwa njia ile ya tarehe 29 Oktoba 2025 na kwamba ulikuwa ni uasi na uovu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ukweli ukishafahamika haijalishi mapokeo yake, ukweli ukiingia moyoni hutafakariwa na ukiona umepotezewa basi jua hauna maslahi kwa uliyemfikia.

Ukweli kwamba watu wanapotea au wanatekwa ikiwa jukumu la usalama wa raia na mali zao likiwa chini ya jeshi la Polisi ambalo tarehe 29 Oktoba 2025, liliwapiga risasi walioandamana kuhanikiza haki hiyo.

Watu walidai mifumo ya uchaguzi iliyohuru waliowadai walidai kuwa uchaguzi ulikuwa huru na tume ilikuwa huru, isipokuwa vyama vyao viliutazama uchaguzi vikagundua kuwa havitatoboa vikaamua kususia uchaguzi.

Tume hiyo ya uchaguzi ilimtangaza mshindi kwa zaidi ya kura 31 milioni kwa asilimia 97, ikijua kuwa baadhi ya vituo ilipofika saa tano tu vilifungwa na baada ya kuzuka vurugu za waandamanaji.

Waangalizi wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na umona wa Afrika walisema kuwa uchaguzi wa Tanzania hakuwa huru wala wa haki tume inapataje uhalali wa kujiita tume huru ya uchaguzi ikiwa ina dosari za wazi.

Tume hii ilianza kulalamikiwa kabla haijanza kazi kutokana na upatikanaji wa wajumbe wake, kuna wateuzi wa rais moja kwa moja na wapo watumishi wa serikali walioitwa watendaji waandamizi wa serikali ndio wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo hawa ni mbadala wa wakurugenzi kwa maama nyingine unaruka najisi ya mkojo unakanyaga kinyesi.

Vijana wa sasa sio vijana wa zamani wale waliokutana na Rais pale katika ukumbi wa JNICC, waliokuwa wakipiga makofi hata walipoambiwa kuwa serikali ilitumia nguvu kubwa sababu ilistahiki.

Vijana wale wa kale walipiga makofi waliambiwa kuwa waliwaacha watoto wao wakaandamane wasilalamike kwa kilichowapata.

Wamesahau kuwa wapo ambao waliuawawa wakiwa nyumbani kwao, wengine walifariki kwa risasi walipokuwa wanaenda dukani.

Wengi walitarajia Rais anakuja na kurasa mpya na kuchana kurasa ya zamani aliyoitaja kuwa imetutia doa ameiacha kura hiyo kuwa ndio ukurasa wa mbele kwa kitabu chetu.

Ujumbe wa haki umemfika umepokelewa na kutafsiriwa tofauti.

About The Author

error: Content is protected !!