December 4, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

PUMA Energy Tanzania yapata tuzo mbili kwenye Consumer Choice Awards

 

PUMA Energy Tanzania imetunukiwa tuzo mbili kubwa kwenye hafla ya mwaka ya Consumer Choice Awards, ambazo ni “Kampuni Inayopendwa Zaidi ya Mafuta na Nishati Barani Afrika” na “Kituo cha Mafuta kinachotoa Huduma kwa Wepesi na Kupatikana kwa urahisi.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ushindi huu wa tuzo mbili unaonesha kwamba PUMA Energy si tu kinara katika huduma za rejareja za nishati hapa Tanzania, bali pia katika bara zima la Afrika.

Tuzo hizi, zilizopigiwa kura na watumiaji pamoja na wataalamu wa sekta, ni uthibitisho wa mkakati wa kampuni katika kutoa bidhaa bora za mafuta na nishati, mtandao mpana wa vituo vya kisasa, na kiwango cha juu cha utoaji wa huduma.

Tuzo ya “Kampuni Inayopendwa Zaidi ya Mafuta na Nishati Barani Afrika” ni uthibitisho wa taswira chanya ya PUMA Energy barani kote Afrika na picha ya uaminifu, weledi wa kiutendaji, na suluhu bunifu za nishati. Tuzo hii inaonyesha imani ambayo mamilioni ya watumiaji, wafanya biashara, na washirika wanaendelea kuwa nayo kwa PUMA Energy katika shughuli zao za kila siku.

Wakati huo huo, tuzo ya “Kituo cha Mafuta kinachotoa Huduma kwa Wepesi na Kupatikana kwa urahisi.” inaonesha ubora wa utekelezaji wa kampuni hapa nchini. PUMA Energy imewekeza kwa uthabiti kwenye maeneo ya kimkakati, miundombinu ya kisasa, na huduma zinazokidhi mahitaji ya madereva wa kisasa wa Kitanzania kuanzia vituo vyenye mwanga wa kutosha, usalama, usafi wa mazingira, malipo ya kidigitali, hadi mtandao mpana unaohakikisha kituo cha PUMA hakiko mbali na mteja.

Mkurugenzi Mtendaji wa PUMA Energy Tanzania, Fatma Abdallah, alisema: “Tunapenda kurudisha shukrani zetu kwa wateja na watumiaji wetu, kwa kutupa sisi nafasi ya kupokea tuzo hizi kubwa. Tuzo hii ya Kampuni inayopendwa zaidi ni mafanikio makubwa yaliyochangiwa na kila mshiriki wa timu ya Puma Enenrgy Tanzania, wauzaji wetu, na wateja wetu wapedwa.

“Tuzo ya Kituo Kinachopatikana kwa Urahisi  ni uthibitisho wa kujitoa kwetu na kuhakikisha kila mteja anayeingia kwenye vituo vyetu anapa huduma bila usumbufu, bidhaa za uhakika na kuondoka akifurahi. Tuzo hizi si mwisho wetu, bali zimekuwa chachu ya kutusukuma kuendelea kutoa huduma za viwango vya juu zaidi”

Mwisho, Mkuu wa Sheria na Masuala ya Ushirika wa PUMA Energy Tanzania, Emmanuel G. Bakilana, alisema, “Tunajitahidi kila mara kuhakikisha mteja yupo katikati ya kila tunachofanya.”

About The Author

error: Content is protected !!