Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikilihusisha shirika hilo na matukio ya kiuhalifu. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Dk. Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini TEC alisema kuwa wakati wa shambulio lake umeme ulikatika na kwamba huo ulikuwa mkakati wa shambulio lake.
Katika taarifa iliyotolewa jana 1 Desemba 2025, na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja kutoka makao makuu ya shirika hilo jijini Dodoma, Tanesco, imeeleza kusikitishwa na taarifa hizo ikisisitiza kuwa hazina ukweli wowote na hazihusiani na majukumu ya shirika katika uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wamesema kukatika kwa umeme huweza kusababishwa na sababu za kiufundi kama hitilafu za dharura kwenye miundombinu au matengenezo yaliyopangwa kwa lengo la kuboresha huduma.
Tanesco, imeeleza kuwa shughuli hizi zote hutekelezwa kitaalamu na kwa taratibu zilizowekwa, hivyo haziwezi kuhusishwa na vitendo vya uhalifu.
Shirika hilo limewataka wananchi kujiepusha kutoa na kusambaza taarifa zisizothibitishwa, kwani zinaweza kupotosha umma na kuathiri taswira ya shirika.
Tanesco, imesisitiza kuwa itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, uadilifu na kuhakikisha huduma ya umeme inaendelea kupatikana kwa uhakika kwa wateja kote nchini.
ZINAZOFANANA
Samia: Oktoba 29 walitaka kupindua dola ninayoiongoza
Kifahamu kilichomo mkutano wa Samia na Wazee wa Dar
Katibu wa Nyerere akosoa mkutano wa Samia na Wazee wa Dar es Salaam