KATIBU Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEF), Padri Charles Kitima, amesema kuwa siku aliyovamiwa na kushambuliwa katika makao makuu ya baraza hilo, Kurasini jijini Dar es Salaam umeme ulikatwa. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Dk. Kitima aliyekuwa akihojiwa na vyombo mbalimbali vya habari leo, tarehe 1 Desemba 2025, amesema kuwa alishangazwa kuona siku na muda alioshambuliwa na kwamba ilikuwa ni mkakati ili auawe.
“Hawa waliokuwa kunivamia kwanza wanazima umeme ili ni uawe mbona hizi mbinu kama kuna mkakati umepangwa hivi baadaye walikuja hawa watu wanaohusika na upelelezi walipokuja kutka kunihoji nikawaambia sitaki lakini niliongea nao baada ya kutoka hospitali”
Dk. Kitima amesema kuwa baada ya matukio hayo kajua kuwa hawa watu wasiojulikana kuwa wapo kweli .
Amedai kuwa hata Padri wa Kanisa hilo aliyedaiwa kujiteka si kweli bali alitekwa na alipuliziwa na kitu usoni kwake “ameeleza siku alivyotekwa alipuliziwa dawa na kabla ya siku ya tukio, alitoa tafakari kuwa Mwanza kuhusu tatizo la usalama akachambua jina moja baada ya jingine katika orodha ya waliotekwa iliyotolea na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
“Taarifa aliyoitoa RPC bila kumhoji yeye kwa sababu kama alikuwa hajatekwa hizo taarifa ameitoa wapi”
Kuhusu hali yake inaendelea kuimarika taratibu “Naendelea kupambana na hali yangu si unajua ukiumizwa kwenye ubongo “.
“sitarejea nyuma nitaongeza zaidi ujuzi , ujuzi wa kufanya kazi zangu hizi za kuongea ”
Dk. Kitima amesema kuwa kuua watu hakutaweza kuwanyoosha na kwamba huwezi kushindana na vijana .
“Tusipouondoa huu uchafu ulioingia kwa kudhani unaweza kunyoosha watu kwa kuuawa tutaharibu nchi vibaya mno huwezi kushindana na vijana,”.
Ametoa wito kuwa Tamko la TEC linalenga kuponya nchi na kuponya nchi ni kukikiri ukweli na anayepaswa kukiri ukweli ni serikali kwa niaba ya wananchi.
ZINAZOFANANA
Vijana wa kike wanachangia asilimia 80 ya maambukizi ya vvu
Tujihadhari na vurugu, tupate maendeleo – Mwigulu
Mangungu awaacha wanachama wa Simba njia panda.