Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres
JINAMIZI la matukio ya 29 Oktoba 2025, bado linaisakama Tanzania na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam …(endelea).
Bunge la Ulaya limepitisha kwa wingi wa kura maazimio tisa (9) yanayoilenga kuifutia Tanzania misaada; kutoutambua uchaguzi mkuu uliyomuingiza Rais Samia madarakani na kutaka kufanyika uchunguzi huru wa mauaji ya raia na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.
Aidha, Wakfu wa Thabo Mbeki, rais mstaafu wa Afrika Kusini, imegoma kutambua uchaguzi uliyofanyika; imetaka kuwapo maridhiano ya kitaifa na kuundwa serikali mpya na shirikishi.
Katika taarifa yake, Wakfu wa Mbeki umesema,
Vilevile, muungano wa mawakili na watetezi wa haki za binadamu, wamefungua malalamiko kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu (ICC), wakitaka mahakama hiyo, kuwachunguza maofisa waandamizi wa serikali, wanaowatuhumu kuhusika na mauaji ya raia na ukatili dhidi ya waandamanaji.
Kamishena Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN), Volker Türk, naye ametoa wito wa kufanyika uchunguzi juu ya mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika wakati wa uchaguzi huo.

Taarifa ya Kamishena huyo inadai kuwa mamia ya waandamanaji na watu wengine waliuawa na idadi isiyojulikana kujeruhiwa au kushikiliwa.
Serikali ya Tanzania, kupitia kwa inakana Waziri wa Mambo ya Nje, Mohamed Thabit Kombo, imekana madai hayo. Imesema, kuzimwa kwa mtandao, kulizingatia maslahi ya taifa.
Kwa mujibu wa UN, “Taarifa za familia zinazosaka wapendwa wao kila mahali kwa kutembelea kituo kimoja cha polisi baada ya kingine na hospitali moja baada ya nyingine ni za kutisha.”
Kamishena wa umoja wa mataifa anasema, “Naomba sana serikali ya Tanzania itoe taarifa kuhusu hatma na mahali walipo wote waliopotea, na kukabidhi miili ya waliouawa kwa wapendwa wao ili wazikwe kwa heshima.”
Anaongeza, “…kuna ripoti kwamba vikosi vya usalama vimeonekana vikiondoa miili kutoka mitaani na hospitalini na kuipeleka kwenye maeneo ambayo hayajajulikana katika jaribio la kuficha ushahidi.”
Naye Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu hali nchini Tanzania kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025 na ripoti za vifo na majeruhi wakati wa maandamano.
Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Stephanie Dujarric, mjini New York, Guterres amelaani vikali vifo hivyo na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za waathirika.

Katibu Mkuu wa UN, amesisitiza umuhimu mkubwa wa kulinda haki za msingi, hasa haki ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza, ikiwemo upatikanaji wa taarifa.
Akatoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kamili na usio na upendeleo kuhusu madai yote ya matumizi ya nguvu kupita kiasi.
Maseneta wa Marekani, wamepuuza matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na wameng’ang’aniza serikali yao, kushinikiza Serikali ya Tanzania, kufanya uchunguzi huru na wazi wa matukio yaliyoripotiwa kutokea kabla na baada ya uchaguzi huo.
Katika azimio lake, lilipotishwa mjini Brussels leo Alhamisi, tarehe 29 Novemba, Bunge la Ulaya limesema limepata ushahidi wa kuwapo matumizi ya nguvu kupita kiasi yaliyofanywa na vyombo vya usalama tangu siku ya uchaguzi, hali iliyosababisha vifo vya maelfu ya watu, majeruhi, raia kukamatwa kiholela, na taarifa za kuwepo kwa makaburi ya halaiki.
Bunge hilo limeilaani serikali kwa kile ilichokiita, “kukanusha ukweli huu licha ya ushahidi kuongezeka.”
Bunge la Ulaya Bunge la Ulaya, limetaka Serikali ya Tanzania kuchukua hatua za haraka na za makusudi kukutana na wadau wa siasa hususani wa vyama vya upinzani ili kutatua ‘matatizo’ yaliyopo na kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi mwingine mpya na wa wazi utakaoakisi misingi ya uhuru na haki.
Kuhusu kiongozi wa upinzani nchini, Tundu Lissu, Bunge hilo limetaka serikali kumuachia mara moja na bila masharti; kumruhusu kupata matibabu, kuonana na familia yake, pamoja na wanasheria wake.
Bunge hilo limetaka Serikali kusitisha mara moja ukamataji holela wa wanachama wa upinzani, waandishi wa habari, waandamanaji na watetezi wa haki za binadamu, kuzuia intaneti na kudhibiti vyombo vya habari.
Rais wa Bunge la Ulaya ameagizwa kupeleka azimio hilo kwa Serikali ya Tanzania, Bunge la Jamhuri ya Muungano, Baraza la Ulaya, Tume ya Ulaya, Umoja wa Afrika, SADC, ACP na Umoja wa Mataifa (UN).
Kuhusu malalamiko yaliyotinga The Hague, nyaraka za mawakili wa waathiriwa wanaoungwa mkono na chama cha wanasheria duniani na chama cha wanasheria wa Madrid, wanadai kuwa kumefanyika mauaji ya holela nchini, pamoja na utekaji nyara, utesaji na vitendo vingine vya vitisho dhidi ya wapinzani wa kisiasa.
Hati ya mahakama, iliowasilishwa pamoja na shirika la Intelwatch la Afrika Kusini tarehe 13 Novemba, inaitaka ICC kuzingatia uhalifu dhidi ya ubinadamu na kutoa hati za kukamatwa kwa Rais Samia na viongozi wake wa vyombo vya usalama.
Wachambuzi wa masuala ya sheria wanasema kuwasilisha maombi ya kutaka ICC kufungulia mashitaka viongozi wa serikali, kunamuweka rais Samia kwenye wakati mgumu zaidi, wakati huu anapoanza muhura wake wa mwisho wa urais.
ZINAZOFANANA
Bunge la Ulaya lapitisha maazimio tisa dhidi ya Tanzania
Wanajeshi wa Marekani wapigwa risasi karibu na Ikulu ya White House
Jeshi lampindua Rais Guinea-Bissau