WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amekutana na Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), na kuwakumbusha wajibu wao wa kuunganisha serikali kimtandao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mkutano na watumishi hao, umefanyika katika ofisi za mamlaka hiyo jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo iliyofanyika jana 24 Novemba 2025, Waziri Kikwete aliambatana na viongozi wengine akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi, Regina Qwaray na Katibu Mkuu Ikulu, Mululi Mahendeka.
Alisema: “Naikumbusha mamlaka kuwa ina wajibu wa kuendelea kuhakikisha inasimamia na kuendeleza kazi ya kuunganisha serikaki kimtandao na kimifumo,” na kuongeza, hiyo itasaidia serikali kuendelea kuwa salama kidigitali.
ZINAZOFANANA
Mwamoto, Kabati walimlilia Lukuvi
Mipango mbioni kuanzisha kituo cha Kimataifa cha huduma za kifedha nchini
William Lukuvi afariki dunia