November 25, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Tanzania inahujumiwa kwa sababu ya rasimali zake -Dk Mwigulu

Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchema amesema matukio yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025, ni hujuma kwa Tanzania ikilenga kuwafitinisha wananchi wagawanyike. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

DK. Mwigulu akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, leo tarehe 25 Novemba 2025, amesema kuwa Tanzania inapigwa vita ya uchumi.

Amesema kuwa hujuma hizo zinafanyika kupitia Watanzania wachache wenye nia ovu ya taifa lao.

Amesema kuwa hujuma hizo ni kama husda dhidi ya rasimali zilizopo nchini; “Watu wanatazama rasimali ndivyo walivyofanya kwa wenzetu walikuwa wanawapa mabomu wao wanachukua rasimali zilipoisha rasimali wakaacha kuwachonganisha, niwahakikishe wale wanaomezea mate Tanzania na wanaotumwa tutailinda Tanzania kwa gharama zozote wala Tanzania haitaendeshwa ka limoti,” amesema Dk. Mwigulu.

Amesema kuwa hujuma hizo zimekuja hivi karibuni baada Tanzania kutaka kuanza mradi wa gesi asilia iliyokuwepo mkoan Lindi (LNG).

“Ni hujuma ya wazi ya kiuchumi dhidi ya Tanzania Miaka yote hakujawahi kutokea wependa Tanzania namna hii baada ya kwamba mradi wa LNG (mradi wa gesi asilia Lindi) utakaofanya Tanzania kuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa wa gesi asilia duniani, eti ndio Watanzania wagawanyike vipande vipande, katika mwaka ambao mradi wa makaa ya mawe na chuma Tanzania ikiwa wazalishaji wakubwa watano wa makaa ya mawe na chuma,” Nchemba

About The Author

error: Content is protected !!