WATU watatu wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya ABC lililokuwa likitoka Iringa kuelekea Dar es Salaam kugongana na basi la Kelvan International lililokuwa likitoka uelekeo wa Morogoro kwenda Songea, ajali iliyotokea eneo la Ng’apa, Mikumi mkoani Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).
Akizungumza kuhusu ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 23 Novemba 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi la ABC, Mussa Mbaga ambaye alijaribu kuyapita magari mengine katika kona bila kuchukua tahadhari, hali iliyosababisha magari hayo mawili kugongana uso kwa uso.
Kamanda Mkama amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu watatu huku majeruhi watano wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mt. Kizito iliyopo Mikumi.
Ameongeza kuwa juhudi za kumtafuta dereva wa basi la ABC zinaendelea, baada ya kukimbia kusikojulikana mara baada ya kutokea ajali hiyo.
ZINAZOFANANA
Tanzania inahujumiwa kwa sababu ya rasimali zake -Dk Mwigulu
Polisi yathibitisha kutoa kwa mauaji ya mtoto wa miaka miwili Mara
Washtakiwa 57 wa uhaini waanza kuachiliwa