NI siku 10 tangu Rais Samia Suluhu Hassan, alivyotangaza waandamanaji walioshtakiwa kwa mashtaka ya uhaini katika mahakama mbalimbali nchini ambao waliingia kwenye maandamano kwa kufuata mkumbo , agizo hilo limeanza kutekelezwa. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Leo tarehe 24 Novemba 2025, Washitakiwa 57 kati ya 61 katika kesi ya uhaini namba 26641/2025 wameachiwa huru leo, Jumatatu tarehe 24 Novemba 2025, na Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilemela, mkoani Mwanza, baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha taarifa kuwa hauna nia ya kuendelea na mashitaka dhidi yao.
Wakili wa Serikali Mwandamizi wa Wilaya ya Ilemela, Safi Amani, amesema mashitaka dhidi ya washitakiwa hao yanaondolewa chini ya Kifungu 92(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), Sura ya 20, marekebisho ya mwaka 2023, kufuatia Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuonesha kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo kwao.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Ilemela, Stella Kiama, amesema washitakiwa wanne waliobaki katika kesi hiyo watarejeshwa mahabusu ya Gereza Kuu Butimba hadi tarehe 1 Desemba 2025, kesi itakapotajwa tena.
ZINAZOFANANA
Wahamiaji haramu 14 wakamatwa Mwanza
Thabo Mbeki: Tanzania inahitaji mwanzo mpya haraka
Ripoti yetu kuhusu Tanzania imezingatia weledi – CCN