SERIKALI ya Ireland na Denmark, zimetaka kufanyika uchunguzi huru kuhusu kinachoitwa, “mauaji ya kiholela na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Tanzania.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa ya serikali ya Ireand iliyotolewa na ubalozi wake jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa inaunga mkono kikamilifu wito wa kufanyika uchunguzi huru nchini, kuhusiana na mauaji ya wakati wa uchaguzi.
“Serikali Ireland inathibitisha msimamo wake wa kuunga mkono kikamilifu wito wa Kamishna wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, kufanyika uchunguzi wa mauaji yanayohusiana na uchaguzi mkuu wa 29 Oktoba na ukiukaji mwingine wa haknchini Tanzania,” imeeleza taarifa hiyo.

Msimamo wa ubalozi huo, umekuja siku moja baada ya Denmark, kutoa wito wa kufanyika uchunguzi wa aina hiyo.
Uidhinishaji huu unafuatia tangazo la awali la Denmark la kuunga mkono kufanyika kwa uchunguzi, na kuongeza kasi ya shinikizo la kimataifa kwa mamlaka za Tanzania kuruhusu uchunguzi huru na kukuza uwajibikaji.
Kabla ya Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa – kutoa wito wa kufanyika uchunguzi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres, alieleza wasiwasi wake kuhusu mauwaji yaliyotokea nchini katika wiki ya uchaguzi mkuu.
Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, matamko kutoka Umoja wa Mataifa yamekuwa yakipuuzwa au kutopewa uzito unaostahili.

Mathalani, kile ambacho kimekuwa kikiendelea katika ukanda wa Gaza, ambapo pamoja na makemeo dhidi ya Israel na tahadhari za mara kwa mara, kutokana na vitendo vyake dhidi ya Wapaelstina, hakuna hatua zozote za muhimu kulingana na taarifa na ripoti za umoja huo.
Bali hiyo, haimaanishi kwamba kauli kutoka UN, hasa kwa viongozi waandamizi kama katibu mkuu na Kamishena wa haki za binadamu, hazina hazina mashiko.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema, “…kwa kile kilichotokea Tanzania, kauli za viongozi hao wa ulimwengu na wito wa serikali nyingine ulimwenguni, zina maana kubwa katika muktadha wa mfumo wa haki katika jumuiya ya kimataifa.”
Kwanza, katika kuweka unyeti juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu na hasa mauwaji ambayo hadi hivi sasa hakuna taarifa kwa umma juu ya kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya washukiwa wakuu wa vitendo hivyo.

Kauli ya katibu mkuu na Kamishna wa Haki za Binadamu zinathibitisha kwamba kilichotokea hakikuwa kidogo cha kuachwa kubaki ndani ya mipaka ya Tanzania pekee; ni kitu kilichostua jumuiya ya kimataifa.
Lakini kwa kuzungumzia mauwaji yale na kutaka uwajibikaji wa waliohusika, UN unapiga muhuri maumivu na vilio vya waathirika na watu wengine walioguswa moja kwa moja na ghasia zilizotokea kana kwamba kusema malalamiko na vilio vyao ni halali.
Aidha, hatua hii ya UN pia inaweka kumbukumbu na rejea ya muhimu ambayo inaweza kutumika katika kuchukua hatua zozote ambazo nchi moja moja au jumuiya ya kimataifa itataka kuchukua.
Hii imeonekana kwa nchi kama Rwanda au Israel ambapo nchi fulani zilipotaka kuchukua hatua kama za vikwazo, walitumia kauli na tafiti za UN kama rejea za uamuzi wao.
ZINAZOFANANA
Machafuko ya 29 Oktoba: Maaskofu Katoliki wataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wawajibike
Meridianbet yaendelea kuwekeza kwa jamii kupitia MRC Rehabilitation Centre
Samia atangaza msamaha kwa waandamanaji