Kampuni ya michezo ya kubashiri inayoongoza nchini, Meridianbet Tanzania, imeendeleza utamaduni wake wa kuwainua watu wanaoishi katika mazingira magumu kupitia miradi ya kijamii (CSR). Katika tukio la hivi karibuni, kampuni hiyo ilitembelea MRC Rehabilitation Centre jijini Dar es Salaam, ikitoa msaada wa vyakula na mahitaji muhimu kama sehemu ya kujitolea kuboresha maisha ya wale wanaopitia changamoto kituoni hapo.
Mchango huo, uliohusisha bidhaa kama unga, mchele, mafuta, sabuni na bidhaa nyingine muhimu, umekuwa zaidi ya zawadi kwani ni alama ya matumaini na uthibitisho kuwa kampuni binafsi zinaweza kuwa chanzo cha faraja na mabadiliko katika jamii. Kwa Meridianbet, kusaidia jamii si tukio la mara moja, bali ni sehemu ya falsafa yao inayojikita katika kuwajali watu.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, mwakilishi wa Meridianbet alisema kuwa kampuni hiyo inaamini mafanikio ya kweli hupatikana pale ambapo biashara inakuwa chanzo cha matumaini kwa wengine. “Kila mwezi tunajitahidi kugusa maisha ya watu wanaohitaji msaada. Tunaamini biashara inapaswa kuacha alama, siyo tu kwenye soko, bali pia kwenye mioyo ya watu,” alisema kwa msisitizo.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Viongozi wa MRC Rehabilitation Centre nao walionesha furaha yao kwa msaada huo, wakieleza kuwa umefika katika kipindi muhimu ambapo kituo kinahitaji rasilimali za kusaidia wagonjwa wanaopata matibabu. “Msaada huu umeonyesha wazi kwamba Meridianbet ni zaidi ya kampuni ya michezo ya kubashiri, ni rafiki wa jamii,” alisema mmoja wa viongozi wa kituo hicho.
Kupitia mpango wao endelevu wa CSR, Meridianbet imejijengea taswira ya kipekee kama kampuni yenye moyo wa utu, inayoweka binadamu mbele ya faida. Kwa kutoa misaada kama hii, kampuni hiyo inaendelea kuimarisha daraja kati ya biashara na jamii, ikionesha kuwa kila dau linaweza kuleta tofauti pale linapowekwa katika matendo ya huruma.
ZINAZOFANANA
Kila sekunde ina thamani na Meridianbet
Samia atangaza msamaha kwa waandamanaji
Watumishi LHRC wadai kukamatwa na Polisi