Dk. Hussein Ali Mwinyi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi, amesisitiza serikali yake itaheshimu maridhiano na kuendesha serikali ya umoja wa kitaifa (SUK). Anaripoti Shamsa Haji, Dar es Salaam … (endelea).
Serikali ya umoja wa kitaifa inatokana na Katiba ya Zanzibar yam waka 1984 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 ambapo ibara ya 39- 42 zimejenga msingi wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Kwa kifupi chama kitachoongoza kwenye uchaguzi kitatoa rais wa Zanzibar huku chama kilichofuata kitatoa Makamu wa kwanza Rais.
“Katika kuendeleza mshikamano na umoja wetu kwa misingi ya katiba yetu serikali yetu itaendeshwa kwa umoja wa kitaifa,”amesema Rais Mwinyi.
ZINAZOFANANA
Heche, Lema, Golugwa na Jacob, waachiliwa kwa dhamana
Uhamiaji kukanusha unyang’anyi wa pasipoti
Serikali yaweka pingamizi kesi ya Heche dhidi ya IGP