November 10, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais Samia awateua Gwajima, Dk. Bashiru kuwa wabunge

Dk. Dorothy Gwajima

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ameteua wabunge sita kuwa wabunge la Jamhuri. Anaripoti Shamsa Haji, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia amefanya uteu huo leo tarehe 10 Novemba 2025 ambapo amewateua, Dk. Dorothy Gwajima, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Dk. Bashiru Ally, Abdullah Ali Mwinyi, Balozi Khamis Mussa Omar na Dk. Rhimo Nyansaho.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Balozi Dk. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi .

Katiba ya Tanzana ya mwaka 1977 ibara ya 66 (1) (e) inampa mamlaka Rais kuteua watu 10 kuwa wabunge wa Jamhuri.

About The Author

error: Content is protected !!