John Heche, Makamu wa Mwenyekiti wa Chadema
WAKILI wa John Heche Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Hekima Mwasipu, amesema kuwa wamefungua kesi Mahakama Kuu wakilishtaki Jeshi la Polisi kwa kumshikilia mteja wake (Heche) kwa muda mrefu nje ya muda ulioelekezwa na sheria. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Heche alikamatwa tarehe 22 Oktoba 2025, akiwa kwenye viunga vya Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam alipokwenda kusikiliza shauri Na.19605 la mwaka 2025 la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu.
Tangu Heche akamatwe hadi leo, tarehe 6 Novemba 2025 zimeshapita siku 15 akiwa mikononi mwa jeshi hilo ambalo mpaka sasa halijamfikisha mahakamani.
Wakili Mwasipu, amesema wamefungua shauri hilo ili kutafuta haki ya Heche.
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Polisi hawaruhusiwi kumshikilia mtuhumiwa kwa zaidi ya saa 48, Heche ameshikiliwa kwa saa 360.
ZINAZOFANANA
Watu 300 waliokamatwa kwenye maandamano Kilimanjaro waachiwa
ACT yatia shaka kifo cha diwani wao aliyekuwa mahabusu
Hatutakubali kubezwa tena – OMO