UCHAGUZI mkuu wa 29 Oktoba 2025, nchini Tanzania, haukikidhi kanuni na viwango vya demokrasia. Ndivyo wanavyoeleza waangalizi wa Umoja wa Afrika (AU), katika ripoti yao, iliyotolewa jana Jumatano, tarehe 5 Novemba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Waangalizi wa AU wamesema, wameshuhudia kanuni za uchaguzi zikikiukwa katika vituo kadhaa vya kupigia kura, ambapo baadhi ya wapiga kura walipatikana na zaidi ya karatasi moja ya kupigia kura.
Aidha, katika baadhi ya vituo mawakala wa vyama vya kisiasa waliondolewa, jambo ambalo limesababisha kuwapo dosari kubwa.
Wakati wa kuhesabu kura, waangalizi wengine waliamriwa kuondoka vituoni, taarifa hiyo iliongeza.
Haya yamejiri wakati ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), iliyoeleza uchaguzi huo ulivurugika.
Hata hivyo, Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
Katika taarifa yake, waangalizi wa Umoja wa Afrika (AU) wameongeza: “Tanzania inapaswa kutoa kipaumbele kwa mageuzi yanayopendekezwa na upinzani ili kushughulikia changamoto za zilizoibuka kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa wiki iliyopita.”
Miongoni mwa marekebisho hayo, ni pamoja na kuwapo uwajibikaji na uwazi wa taasisi za serikali; ujumuishwaji na kuheshimu maoni tofauti ya wadau wa kisiasa na wananchi na ushiriki wa wananchi katika michakato ya kisiasa na ya uchaguzi,
Marekebisho mengine, ni ulinzi na heshima kwa haki za binadamu katika ngazi zote za utawala.
Ujumbe huo wa AU pia imeeleza kutamaushwa na vifo vilivyotokana na maandamano ya baada ya uchaguzi, na kutoa rambirambi kwa familia zote zilizoondokewa na wapendwa wao.
Umetoa wito kwa mamlaka husika kuchunguza matukio hayo kwa uwazi, na kuhakikisha haki inatendeka kwa wote walioathirika.

Juzi Jumanne, tarehe 4 Novemba, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB) imesema, itaanzisha uchunguzi wa kina kufuatia maandamano yalioshuhudiwa wakati wa uchaguzi huo na kusababisha uharibifu wa mali na vifo vya raia.
Rais Samia Suluhu alitangazwa mshindi katika uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba 2025, lakini Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye kiongozi wake Tundu Lussi anazuiliwa jela kwa tuhuma za uhaini, kilipinga matokeo hayo na kudai kuwa uchaguzi huo kama kejeli kwa demokrasia.
Naye John Heche, naibu mwenyekiti wa chama hicho, anakishikiliwa na jeshi la polisi nchini Tanzania, wakimtuhumu kwa makosa ya ugaidi.
Heche aliyekamatwa wiki mbili zilizopita na kusafirishwa hadi mkoani Dodoma na baadaye kurejeshwa jijini Dar es Salaam, anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kutoka sasa.
ZINAZOFANANA
Watu 300 waliokamatwa kwenye maandamano Kilimanjaro waachiwa
Hatutakubali kubezwa tena – OMO
Mawakili wa Heche walishtaki Jeshi la Polisi