October 25, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mahakama: Hakuna ushahidi Polepole anashikiliwa na IGP na wenzake

Humphrey Polepole

 

MAHAKAMA Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri la maombi ya amri ya kumfikisha mahakamani au kumwachia kwa dhamana, Humphrey Polepole, ikieleza hakuna ushahidi kuwa wajibu maombi ndio waliomchukua. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Shauri hilo ambalo wajibu maombi ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Mwanasheria Mkuu wa serikali (AG), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Upelelezi Kanda ya Dar es Salaam (ZPC) na Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Saalam (ZCO).

Uamuzi huo ulioandikwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salma Maghimbi, aliyesikiliza shauri hilo umesomwa leo tarehe 24 Oktoba, 2025 na Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Livin Lyakinana.

Mahakama imesema kutokana na mazingira halisi hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba wajibu maombi wanamshikilia Polepole.

Kibatala amesema kuwa imekuwa ngumu kuithibitisha mahakamani ni nani aliyemchukua Polepole kutokana na mazingira ya watu kuchukuliwa kwa kuwa hawajitambulishi kwa majina au vyeo vyao.

Hata hivyo Wakili Kibatala amesema tayari ameshakata Rufaa kwa ajili ya kuomba mapitio ya mahakama juu ya shauri hilo.

About The Author

error: Content is protected !!