October 21, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mtoto wa Aboud Jumbe afariki dunia

 

MUSSA Aboud Jumbe, mtoto wa aliyekuwa Rais wa pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Jumanne tarehe 21 Oktoba 2025. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Marehemu Mussa Aboud Jumbe aliwahi, amekutwa na mauti huko nyumbani kwao Migombani, Unguja.

Wakati wa uhai wake, Mussa Aboud Jumbe, aliwahi kuhudumu kama Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar, kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na rais wa sasa wa Visiwa hivyo, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Mwaka 2020, alikuwa miongoni mwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania uteuzi wa chama chake kwa ajili ya kugombea urais wa Zanzibar.

Mwili wa marehemu Mussa unatarajiwa kuzikwa leo hii tarehe 21 Oktoba 2025, saa 10:00 jioni mjini Unguja.

Aliyekuwa rais wa pili wa Zanzibar – Aboud Jumbe Mwinyi – ambaye alivuliwa nyadhifa zote serikalini na ndani ya CCM kutokana na kutofautiana na chama hicho katika suala la muundo wa Muungano, alifariki dunia, tarehe 14 Agosti 2016.

Alikuwa rais wa Zanzibar kati ya mwaka 1972 hadi 1984, baada ya kifo cha rais wa kwanza wa Visiwa hivyo, Abeid Amaan Karume, aliyeuawa kwa kupigwa risasi.

About The Author

error: Content is protected !!