
Padri Charles Kitima
BARAZA la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), limekanusha taarifa inayosambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa ni tamko la baraza hilo kuhusu amani kwa Taifa kuelekea siku ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba, 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salasm … (endelea).
Taarifa ya kukanisha tamko hilo imetolewa jana tarehe 13 Oktoba 2025 Katibu Mkuu wa TEC, Padri Dk.Charles Kitima, akisema kuwa kanisa hilo halijahusika na
utoaji wa taarifa hiyo
“Tunapenda kuwatangazia waumini na Watanzania wote kwa ujumla, kuwa waraka huo haukutolewa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania,” Dk. Kitima
Tamko lilikonushwa na TEC lilisamba tangu tarehe 11 Oktoba likidai kuwa baraza linatoa wito kwa waumini wa Katoliki nchini kutojihusisha katika shughuli ambazo zinaweza kuliingiza Taifa katika machafuko.
ZINAZOFANANA
Ilala wafanya dua kumuombea Samia, Tanzania
John Heche ateta na Marando
Mgombea udiwani Kinyerezi ajinadi kuwa mtu wa vitendo zaidi