MAHAKAMA Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemhukumu Suleiman Kwata adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya makusudi dhidi ya Editha Charles, mfanyakazi wa ndani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa hukumu hiyo, tukio hilo lilitokea tarehe 6 Julai 2022, katika eneo la Kimara Temboni, Wilaya ya Ubungo.
Mahakama imeeleza kuwa mshtakiwa, ambaye alikuwa jirani wa marehemu, alimuua Editha kwa kumchoma kisu shingoni baada ya kushirikiana naye kuvunja kibubu na kuiba fedha za mwajiri wake kiasi cha Sh. 16 milioni.
Imeelezwa kuwa wakati wakiendelea kufanya uhalifu huo, mshtakiwa alidaiwa kuingiwa na tamaa ya ngono na kutaka kumwingilia kimwili Editha. Alipokataa, alimshambulia kwa nguvu na kumbaka.
Tukio hilo lilimkasirisha marehemu, ambaye alimtishia kumfichua kwa mwajiri wake. Hapo ndipo mshtakiwa alipomchoma kisu na kusababisha kifo chake.
ZINAZOFANANA
Siku ya Kimataifa ya Wanawake 2026 yasherekewa kwa Kishindo- Kilombero Sugar
Dk. Nchimbi ataka wizara zishirikiane kuimarisha uhifadhi wa mazingira
Jaji Mutungi akutana na Mwakilishi wa UN