
RAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wapya kuongoza taasisi zinazohusika na uendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo haraka nchini UDART. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hatua hiyo imekuja baada ya vurugu zilizotokea jana taerehe 1 Oktoba 2025, katika baadhi ya vituo vya Mwendokasi jiji Dar es Salaam, ambapo wananchi wanaosadakika kuwa ni abiria, kuanza kurusha mawe baadhi ya mabasi ya mwendokasi wakidai huduma hiyo kuwa mbovu na kushindwa kusafiri kwa wakati.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi, na kuwasilishwa na Sharifa Nyanga, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, leo tarehe 2 Oktoba 2025 jijini Arusha, walioteuliwa ni Said Tunda, ambaye ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART). Anachukua nafasi ya Athumani Kihamia ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Aidha Pius Ng’ingo, ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART). Anachukua nafasi ya Waziri Kindamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo uteuzi huu unaanza mara moja.
ZINAZOFANANA
Watatu wakamatwa vurugu mwendo kasi
ZEC: Watakaopiga kura Z’bar hawa hapa, 8,325 hawana sifa
OMO aanza ziara ya siku saba Pemba