
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara, John Heche, ameingia mjini Nyakahanga, wilayani Karagwe, mkoani Kagera, kuhudhuria mazishi ya Benjamin Jacob Bagonza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).
Heche ameungana na mamia ya viongozi, waumini na mamia ya wananchi, katika ibada hiyo ya mazishi ya Benjamin Bagonza, aliyefariki dunia Jumatano iliyopita, tarehe 23 Septemba mwaka huu.
Mzee Benjamin Jacob Bagonza, alikuwa Baba mzazi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza.
Shughuli hiyo ya kuaga mwili imefanyika nyumbani kwa marehemu, huku viongozi hao wakimfariji Askofu Bagonza na familia yake katika kipindi hiki kigumu.
Mzee Bagonza alifariki dunia tarehe 23 Septemba 2025, katika hospitali ya Nyakahanga, wilayani Karagwe.
Heche aliwasili Karagwe jana Ijumaa, tarehe 27 Septemba 2025.
Tunamuombea Mzee Benjamin Bagonza apumzike kwa amani. Familia ya Kanisa na Watanzania wote wawe na moyo wa uvumilivu na subira.
ZINAZOFANANA
Tanesco, wadau wakutana kujadili mikakati ya kulinda vyanzo vya maji Bwawa na Nyerere
Polisi Kigoma waanza uchunguzi ukusanyaji wa vitambulisho vya kura
Meridianbet yatoa vifaa kinga kwa watu wenye ulemavu wa ngozi