
JESHI la Polisi Mkoa wa Kigoma limetoa taarifa kwa umma likieleza kuwa linafanya uchunguzi wa tuhuma zinazowahusisha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaodaiwa kuhusika katika kukusanya na kuandikisha namba za vitambulisho vya kupigia kura vya wananchi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Kigoma Kaskazini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).
Uchunguzi huo unahusu vitendo vilivyofanyika kwenye kata za Mwandiga, Kagunga, Simbo, Mkigo, Kagongo na Kidawe, na Polisi wamesisitiza kuwa endapo utabainika ukweli wa tuhuma hizo, hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024.
Aidha, Jeshi la Polisi limewaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kushirikiana kwa kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia kubaini ukweli, huku likiahidi kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo hivyo vya kinyume cha sheria.
ZINAZOFANANA
Tanesco, wadau wakutana kujadili mikakati ya kulinda vyanzo vya maji Bwawa na Nyerere
Baba Mzazi wa Askofu Bagonza kuzikwa leo
Uchaguzi mkuu ujao: Kupata au kupatwa?