
KATIKA kuendeleza dhamira yake ya kuwajibika kwa jamii, Meridianbet imefanya zoezi maalum la kugawa vifaa kinga kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), ikiwa ni hatua ya kuwalinda dhidi ya madhara ya mionzi ya jua.
Kupitia tukio hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam, kampuni hiyo iligawa kofia na miwani ya jua kwa walengwa, vifaa vilivyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu ili kusaidia kulinda ngozi na macho dhidi ya miale mikali ya jua. Zoezi hili limebeba lengo la kuimarisha afya, usalama na ustawi wa kundi hili maalum ambalo mara nyingi hukumbwa na changamoto za kiafya kutokana na mazingira ya joto kali.
Mwakilishi wa Meridianbet akieleza kwa msisitizo alisema “Tunatambua kuwa jamii ni msingi wa kila tunachofanya. Watu wenye ulemavu wa ngozi wanakumbana na changamoto nyingi, na sisi tumechagua kuwa sehemu ya suluhisho. Tunatoa msaada huu si kwa maneno, bali kwa vitendo.”
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi. Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Wanufaika wa msaada huo walionesha furaha na kutoa shukrani kwa Meridianbet kwa kuwakumbuka. Wengi walieleza kuwa vifaa hivyo vitawasaidia kuishi kwa ujasiri zaidi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii bila hofu ya madhara ya jua.
Hatua hii ni sehemu ya mpango mpana wa Meridianbet wa kusaidia jamii kupitia miradi ya kijamii inayogusa sekta za afya, elimu na mazingira. Kampuni inaendelea kuthibitisha kuwa uwajibikaji kwa jamii ni sehemu ya utambulisho wake.
ZINAZOFANANA
Tanesco, wadau wakutana kujadili mikakati ya kulinda vyanzo vya maji Bwawa na Nyerere
Baba Mzazi wa Askofu Bagonza kuzikwa leo
Meridianbet Bonanza imefika, burudani mpya kabisa!