
MAHAKAMA Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imeyatupa mapingamizi mawili yaliyowekwa na Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika kesi yake ya uhaini. Anaripoti Kevin Mwaipungu, Dar es Salaam …(endelea).
Akisoma uamuzi huo leo Jumatatu, tarehe 22 Septemba, Jaji Dastan Ndunguru, ameeleza kuwa mahakama inakubaliana na hoja ya waendesha mashitaka, ni sahihi na imeandaliwa kwa mujibu wa sheria.
Kesi hiyo Na. 16905/2025, imekuja mahakamani leo, kwa ajili ya kutolewa uamuzi mdogo, kuhusiana na mapingamizi yaliyowekwa na Lissu, kuhusu ubovu wa hati ya mashtaka na maelezo ya mashahidi (witness statement). Alisema, maelezo hayo, “yamechukuliwa kinyume cha sheria.”
Akisoma uamuzi huo wa mahakama, Jaji Ndunguru alisema, anakubaliana na hoja za mawakili wa serikali, kwamba hati inayopelekwa Mahakama Kuu ndio hati halisi na ndio mshitakiwa anasomewa wakati shauri lake linapoanza kusikilizwa, na kwamba hati ndiyo iliyotumika Kisutu.
Aliendelea kueleza kuwa hati ambayo imeletwa hapa Mahakama Kuu haijawahi kubadilishwa na haina marekebisho yoyote.
Aidha, mahakama hiyo imetupa pingamizi lingine la Lissu kuhusu maelezo ya mashahidi kuchukukuliwa kinyume na sheria kwa kusema, kuwa jambo hilo halikupaswa kuletwa kwa sasa kwa kuwa limeshatolewa uamuzi.
Lissu aliwakilisha mapingamizi hayo mara baada ya kusomewa mashitaka, kufuatia kutupiliwa mbali pingamizi lake la awali juu ya mapungufu ya kisheria yaliohusu tararibu za komito kwenye, iliyosomwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Baada ya hatua hiyo, mahakama ilitarajiwa kuanza kusoma mashitaka dhidi ya mwanasiasa huyo machachari nchini.
ZINAZOFANANA
Rostam ni mfano bora wawekezaji ndani na nje ya nchi-TCCIA
ACT tutavunja Tume ya Uchaguzi, tutaunda upya Jeshi la Polisi
Kesi ya Lissu kuanza kutolewa ushahidi Oktoba 6, Samia atajwa