
Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omari
VIONGOZI wa madhehebu ya kidini nchini, wamefanya matembezi ya amani leo Jumamosi, tarehe 20 Septemba, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
“Viongozi wa dini zote, wanafanya matembezi ya amani na sio kufanya uchawa. Ni kuliombea taifa amani, ili izidi kudumu kwenye taifa hili,” ameelza Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omari.
Matembezi hayo yameanzia viwanja vya Mnazi Mmoja hadi viwanja vya mashujaa, kuelekea siku ya Amani Duniani ya 21 Septemba ya kila mwaka.
Hata hivyo, kiongozi huyo hakuzungumzia suala la haki, linalotajwa na wachambuzi wa masuala ya demokrasia, kuwa ndio msingi mkuu wa taifa kuwa na amani.
ZINAZOFANANA
Rostam ni mfano bora wawekezaji ndani na nje ya nchi-TCCIA
Changamoto za afya barani Afrika zitatatuliwa na CDC
ACT tutavunja Tume ya Uchaguzi, tutaunda upya Jeshi la Polisi