
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wakubwa kutoka kwenye makampuni na taasisi mbalimbali (Corporates) wa jijini Mwanza ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo huku ikitangaza dhamira yake ya kuanzisha dawati maalum la wataalam wabobevu katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo madini, kilimo na uvuvi litakaoisaidia benki hiyo kubuni huduma mbalimbali za kibenki mahususi kwa wadau sekta hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).
Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo mwisho wa wiki jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa NBC, Elvis Ndunguru, pamoja na kuwajengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma mbalimbali mpya za benki hiyo alisema ujio wa dawati maalum la wataalam wabobevu kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi utasaidia benki hiyo kuwa karibu zaidi na wadau wa sekta hizo kwa kubuni huduma zinazoendana na mahitaji halisi ya wadau hao.
“Huu ni muendelezo tu wa matukio kama haya, tumekuwa tukitumia fursa kama hizi kujadili na wateja wetu namna tunavyoweza kuboresha huduma zetu kulingana na mahitaji yao. Tukiwa kama muhimuli muhimu wa utoaji wa huduma za kifedha nchini, NBC tunatambua umuhimu wa utoaji wa huduma bora kwa wateja na kukuza ushirikiano kati yetu na wateja wetu. Hii inasababishwa na mabadiliko yanayotokana na ubunifu na maendeleo ya kiteknolojia.’’ alisema Ndunguru.
Aidha, kupitia mpango huo benki hiyo imekuwa ikielezea mikakati yake mipana inayolenga kuwahudumia kwa ufanisi zaidi wateja hao, kuwajengea mitandao ya kibiashara miongoni mwao sambamba na kuwasogezea huduma za kibenki karibu zaidi huku huduma ya NBC Connect ikitajwa kama suluhisho muhimu katika kuwasogezea huduma za kibenki wateja hao wakubwa yakiwemo mashirika na kampuni binafsi, pamoja na taasisi za serikali.
“Tunaamini kuwa msingi wa huduma za kipekee ni kuelewa mahitaji na matakwa ya wateja wetu, ziara hizi zinatupatia mitazamo au maono yatakayosaidia kuwa wabunifu na kuboresha uzoefu wa kibenki kwa ujumla. Kupitia matukio kama haya tuliweza kugundua mahitaji halisi ya wateja wetu kutoka sekta ya biashara na tukaweza kubuni huduma zinazojibu maswali yao.
“Sasa tunakwenda kufanya hivyo hivyo kwa wadau wa sekta nyingine muhimu zikiwemo sekta za madini, kilimo na uvuvi ili tuendelee kuja na huduma stahiki kwao ikiwemo mikopo, bima na elimu zaidi kuhusu uendeshaji wa kisasa wa shughuli zinazohusiana na sekta hizo.” aliongeza Ndunguru.
Aidha, Ndunguru alitaja baadhi ya mambo muhimu ambayo benki hiyo imekuwa ikiyazingatia katika kukuza ushirikiano na taasisi za kibiashara hapa nchini kuwa ni pamoja na utoaji wa suluhisho zenye ubunifu katika huduma za kifedha, ubunifu wa kiteknolojia, ubia wa kimkakati, kukuza ukuaji wa uchumi pamoja na uwajibikaji kwa jamii huku kipaumbeke kikiwekwa zaidi kwenye masula ya elimu, afya na uhifadhi wa mazingira.
Hafla hiyo pamoja na wateja pia ilihusisha uwepo wa maofisa wengine waandamizi wa benki ya NBC kutoka mikoa tofauti ya Kanda ya ziwa na Makao makuu ya benki hiyo akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki hiyo, Msafiri Shayo.
Wakizungumzia hatua hiyo baadhi ya wateja wa benki hiyo mkoani Mwanza wameipongeza benki ya NBC kwa hatua hiyo muhimu huku wakionesha kuvutiwa zaidi na huduma ya NBC Connect.
“NBC Connect imerahisisha sana maisha yetu hasa kwenye upande wa miamala na namna ya upatikanaji wa huduma za kibenki. Jukwaa hili la kidigital maalumu kwa ajili ya taasisi na biashara kubwa linarahisisha zaidi ufanyaji wa miamala ikiwemo kufanya malipo ndani ya nchi kwa TISS ambapo kwasasa tunaweza pia kufanya malipo ya nje kwa urahisi na usalama zaidi,’ alisema mmoa wa wateja hao Nyanjige Ngambeki kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kauli iliyoungwa mkono na Rajab Kinande, Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa.
ZINAZOFANANA
Hospitali ya Kifuma yanufaika na ujio wa Meridianbet
ATCL yatangaza safara ya Dar-Lagos kwa dola 850
Meridian Bonanza inaleta mlima wa bahati kwa wabashiri wote