September 10, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kesi ya mgawanyo mali Chadema yanaendelea kunguruma

John Mnyika, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema

 

KESI ya mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Visiwani na wenzake wawili, dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema na katibu mkuu wa chama hicho, imeendelea kusikilizwa mahakamani, leo tarehe 10 Septemba. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mahakama wakati wa kuhairisha shauri hilo, kesi imekuja mahakamani kwa ajili ya kusikiliza ombi la wadai la kutaka kupewa taarifa ya mali za chama hicho.

Kesi hiyo, inasikilizwa na Jaji Hamid Mwanga, katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

Mbali na Said Issa, wadai wengine kwenye shauri hilo, ni Maulida Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis, waliokuwa wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Chadema.

  • Endelea kufuatilia MwanaHALISI Digital kwa taarifa zaidi.

About The Author

error: Content is protected !!