July 2, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Tundu Lissu apinga kesi yake kuahirishwa tena

 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayekabiliwa na kesi ya uhaini, amepinga vikali ombi la upande wa mashtaka la kutaka kesi hiyo iahirishwe tena kwasababu ya upelelezi haujakamilika, akidai hakuna hoja ya msingi inayowasilishwa kuhalalisha kuchelewesha kwa shauri hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu amepinga ombi hilo leo, tarehe 1 Julai, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakati kesi ikiendelea mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Franko Kiswaga .

Mwanasiasa huyo amedai kuwa ana haki ya kusikilizwa mbele ya mahakama huru na kukosoa kitendo cha serikali kuchelewesha mchakato huo na kuitaka Mahakama iagize kesi yake ipandishwe Mahakama Kuu.

Upande wa Jamhuri kupitia kwa Wakili wa Serikali Mkuu ulikiri kuwa faili la kesi hiyo limeshapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya uamuzi, lakini bado haijafahamika iwapo litatolewa uamuzi wa kuipeleka Mahakama Kuu au kufutwa kupitia hati ya Nolle Prosequi.

Nolle Prosequi ni hati ya kufuta mashitaka ya Mwendesha mashtaka (DPP). Hati hii hutolewa na DPP akieleza kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi na hivyo kuiomba mahakama kufuta mashtaka dhidi ya mtuhumiwa ama watuhumiwa.

About The Author

error: Content is protected !!