MAKADINALI kutoka kwenye kanisa la Sistine huko Vatican, wamemchagua Kardinali Robert Fancis Prevoat kutoka nchini Marekani kuwa kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki Duniani (Papa). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kardinal Robert mwenye umri wa miaka 69, atafahamika kama Papa Leo XIV, kufuatia kuchagua jina hilo.
Kardinalo huyo, anatokea Chicago nchini Marekani, na hadi kuchaguliwa kwake alikuwa akihudumu kama mkuu wa Dicastery wa kanisa kwa Maaskofu.
Prevost ametumia muda wake mwingi akitumikia nchini Peru, na ana uraia wa Marekani na Peru.
ZINAZOFANANA
UNDP, Uingereza watoa 70mil kuimarisha Biashara Bunifu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu
Mojtaba Khamenei ndiye mrithi wa Ayatollah Ali Khamenei, Iran
RITA yatoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa jengo la kituo cha watoto wenye uhitaji Dar