May 1, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

John Mrema avuliwa uanachama Chadema

John Mrema

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemvua uanachama John Mrema aliyekuwa Mkurugenzi wa Uenezi wa Chadema na ambaye sasa anajitambulisha kama Msemaji wa G55. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Kupitia barua iliyosainiwa na Solomani Kagaruki kwa niaba ya Katibu wa Tawi la Chadema Bonyokwa, imemvua uanachama Mrema mara baada ya kamati tendaji kijiridhisha kuwa alidharau mamlaka ya nidhamu ya chama hicho.

Barua hiyo iliyosambaa mitandaoni leo tarehe 30 Aprili 2025, saa 12 Jioni imeeleza kuwa tawi hilo lilimpa Mrema barua ya wito ya tarehe 16 Aprili 2025 badala yake Mrema aliipuuza barua hiyo kwa kuamua kugoma kufika mbele ya Kamati Tendaji na kuichapisha kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha kamati hiyo iliendelea kueleza kuwa, Mrema alikaidi na kuheshimu miiko, tamaduni na misingi ya chama, kwa kupinga misimami na programu za chama katika mkutano wake alioufanya kwa waandishi wa Habari tarehe 22 Aprili 2025.

Barua hiyo ilinukuu Mamlaka ya Tawi hilo kufanya hivyo kuwa ni ibara ya 5.4.3 ya Katiba ya Chama hicho.

Baada ya makosa hayo mawili kamati hiyo ilifikia maamuzi kuwa Mrema amepoteza sifa ya kuwa mwanachama wa Chadema kwa kuvuliwa rasmi uanachama licha ya kuwa na fursa ya kukata rufaa.

About The Author

error: Content is protected !!