April 30, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mwanza mbioni kuzalisha vyanzo vipya vikubwa vya kodi

 

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Saidi Mtanda amsema kutokana na miradi mikubwa ya kimkati inayoendelea mkoani humo anatajia vyanzo vipya vya kodi vitazaliwa na kuifanya mwanza kuwa na mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Mtanda, amesema hayo leo Aprili 30, 2025 alipokutana na ujumbe wa Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ukiongozwa na Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano, Richard Kayombo walipofika kujitambulisha wakati wa zoezi la Elimu ya Mlipakodi mlango kwa mlango kwa lengo la kuelimisha wafanyabiashara katika maeneo yao ya biashara sambamba na kusikiliza changamoto zao.

Mtanda ameeleza kuwa, mkoa mwanza umekuwa miongoni mwa mikoa minne bora inayochangia kiasi kikubwa katika pato Ghafi la taifa (GDP) kwa asilimia 7.2 ambayo inatokana na ulipaji mzuri wa kodi kwa walipakodi wa mkoani hapo mpango ukiwa ni kufikia mchango wa asilimia 10 baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR), upanuzi wa bandari na ununuzi wa Meli na vivuko na ujenzi wa Daraja la Magufuli.

“Mkoa wetu kwa sababu ya ulipaji mzuri wa kodi unachangia Pato Ghafi la Taifa (GDP) kwa asilimia 7.2 na matarijio yetu ni kwenda hadi asilimia kumi mpaka kufikia 12 baada ya miradi inayochochea uchumi kukamilika kama vile Trani ya umeme (SGR) na Upanuzi wa bandari,” amesema Mtanda.

Pia, Mtanda amewashukuru walipakodi wa mwanza kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kuwataka kuendelea kulipakodi vizuri, akiwataka waendelee kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kukamilisha miradi inayoendelea na kuweza kuanzisha mipya.

Wafanyabiashara hao pia wamehimizwa kukahakisha wanatoa risiti kwa kila mauzo wanayoyafanya bila ya kudai na bila ya kushurutishwa na wananchi kudai risiti hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano, Richard Kayombo amesema lengo la zoezi la elimu kwa Mlipakodi mlango kwa mlango ni kuweza kuwafikia wafanyabiashara katika maeneo yao ili kuwafikishia elimu ya kodi sambamba na kusikiliza changamoto zao kwa sababu kuna baadhi ya wafanyabiashara hawahudhurii semina za kodi hivyo wanaweza kupatikana kwa kuwatembelea katika maeneo yao ya biashara.

About The Author

error: Content is protected !!