
KAMA ilivyo kawaida ya mabingwa wa ubashiri Tanzania, Meridianbet kurejesha kwenye jamii, leo hii waliamua kuwageukia wakazi wa Mbezi Juu na kutoa msaada wa vifaa vya usafi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa nia ya kuinua huduma za afya katika jamii, kampuni ya michezo ya kubashiri ya Meridianbet imeendelea kusimamia wajibu wake wa kijamii kwa vitendo kwa kukabidhi msaada wa vifaa vya usafi katika Kata ya Mbezi Juu jijini Dar es Salaam.
Msaada huo umekuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo huku shukrani zikiwa kubwa sana baada ya kupokea vifaa hivyo vya usafi kama vile Dustbins(mapipa ya usafi), glovu za usafi, Reflectors kwa viongozi wa mtaa, maafisa usafi pamoja na wawakilishi wa wananchi ambaye alikuwepo hapo.
Jumamosi ya leo chukua mzigo wako mapema ambapo mechi kibao zipo kwaajili yako siku ya leo. Suka jamvi lako la ushindi leo na ubashiri hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Keno, Poker, Roullette, Keno, na mingine kibao.
Msafara huo wa kufika Mbezi Juu kwaajili ya kutoa vifaa vya usafi kama kawaida Nahodha wao alikuwa si mwingine bali ni Afisa Mahusiano wa Meridianbet Bi Nancy Ingram ambaye alipokelewa vyema kabisa na Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Anna Lukindo.
Baada ya kutoa vifaa hivyo, Nancy alisema kuwa, “Meridianbet tunaamini kuwa usafi ni afya, na afya ni msingi wa maendeleo ya jamii. Kupitia zoezi hili, tunataka kutoa hamasa kwa jamii kushiriki kikamilifu katika kulinda mazingira yao. Tunatambua jukumu letu kama sehemu ya jamii, na hii ni hatua mojawapo ya kuonesha kuwa tunajali,”
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mbezi Juu ameishukuru Meridianbet kwa moyo wa kizalendo na ushirikiano wao katika kuunga mkono juhudi za serikali za mitaa katika kuhakikisha mazingira yanabaki kuwa salama, safi, na yanayovutia.
“Huu ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali katika kuhakikisha tunalinda afya na hadhi ya mazingira ya wananchi wetu. Tunatoa wito kwa kampuni nyingine kuiga mfano huu,” amesema Mh. Anna Lukindo.
Vifaa vilivyotolewa vitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Mbezi Juu ili kusaidia ukusanyaji bora wa taka, kulinda usalama wa watoa huduma za usafi, na kuhimiza uwajibikaji wa pamoja katika kutunza mazingira.
Meridianbet inasisitiza kuwa itaendelea kurejesha kwenye jamii, kwani bila jamii wao si kitu, hivyo pia wanawasihi watu wengine na kampuni zingine kuiga mfano kutoka kwao kwani wenye uhitaji ni wengi sana.
ZINAZOFANANA
Chadema: Tundu Lissu yupo gerezani Ukonga
Serikali yajivunia mafanikio sita ya TASAF
Dk. Kimei aweka rekodi ya utendaji Vunjo