April 16, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dk. Mpango: Tuweke mikakati ya kukuza mapato ya ndani

 

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amesema hali ya ulipaji wa kodi nchini inatutaka kujipanga zaidi kwa kuweka mikakati madhubuti ya kukuza mapato ya ndani. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza hii leo tarehe 15 Aprili 2025 katika Kongamano la kodi na uwekezaji kitaifa, Dk. Mpango amesema pamoja na jitihada kubwa ambazo serikali imefanya ili kuongeza mapato bado hali ya ulipaji kodi nchini inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Kwa mujibu wa Dk. Mpango uwiano wa pato la Taifa umekuwa kwa kasi ndogo kwa zaidi ya miongo miwili kutoka asilimia 12 mwaka 2001/2002 hadi asilimia 14.9 mwaka 2024/2025 ikiwa ni kiwango cha chini ikilinganishwa na wastani wa  asilimia 18.6 kwa nchi za Afrika kusini mwa janga la sahara.

Dk. Mpango ameeleza kuwa ukusanyaji wa mapato ya kodi kwa mwaka 2023/2024 yameshuka kutoka asilimia 126 hadi asilimia 74 wakati sehemu kubwa za halmashauri zikiwa zimeshindwa kusimamia na kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato uliowekwa.

Amesema, “licha ya mpango, taratibu na sera zilizowekwa na serikali bado kuna changamoto za ukusanyaji wa mapato ya ndani, wigo mdogo wa walipa kodi, kiwango kidogo cha ujumuishi wa huduma za fedha na uwepo wa utoroshaji wa fedha.”

Aidha ametoa wito kwa washiriki wa kongamano hili kutoa mchango wa mawazo ili kusaidia kuwepo kwa utawala bora katika mfumo wa kodi, kutanua wigo wa kodi hasa katika sekta ya kilimo na zisizo rasmi.

About The Author

error: Content is protected !!