
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kurejea kwa huduma ya ununuzi wa tiketi za treni kupitia mtandao baada ya kukabiliwa na hitilafu ya mfumo wa malipo ya Serikali, maarufu kama Government Electronic Payment Gateway (GePG). Anaripoti Mwandishi Wetu. Dar es Salaam …. (endelea).
Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa TRC, Fredy Mwanjala shirika hilo limeeleza kuwa changamoto hiyo ilianza usiku wa kuamkia leo tarehe 5 Aprili 2025 na ilisababisha baadhi ya wasafiri kushindwa kupata namba za malipo (control number) kwa ajili ya kununua tiketi za treni za kisasa (SGR).
“Shirika linaarifu umma kuwa hali ya upatikanaji wa tiketi kwa njia ya mfumo wa GePG imerejea kama kawaida,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
TRC imetoa pole kwa abiria wote waliokumbwa na usumbufu uliotokana na hitilafu hiyo ya muda mfupi na kuahidi kuendelea kuboresha huduma zake ili kuhakikisha huduma zinapatikana bila vikwazo.
ZINAZOFANANA
Maadhimisho ya Nne ya Lugha ya Kiswahili yapokewa kwa bashasha Harare, Zimbabwe
Msitumie kalamu zetu kuligawa taifa – Biteko
Siamini ‘sana’ dhana ya uandishi wa katikati – Prof. Mkumbo