
Magari ya Shirika la Posta
MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, ameeleza kuwa Shirika la Posta nchini (TPC), limepata hasara ya Sh. 23.63 bilioni, ikilinganishwa na hasara ya Sh. 1.34 bilioni, katika mwaka uliuopita. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Katika ripoti yake yam waka, aliyoitoa leo, jijini Dar es Salaam, CAG Kichere amesema, shirika hilo limeshuka kwa mapato kwa asilimia 20 na limeongezeka gharama za uendeshaji kwa 46 asilimia.
“Shirika hili, limetumia kiasi cha Sh. 3.36 bilioni, ikiwa ni ruzuku kutoka serikali kuu. Bila rukuzu hiyo, hasara ya shirika ingefikia Sh. 26.96 bilioni,” amefafanua CAG.
Katika mwaka wa fedha wa fedha 2022/23, CAG Kichere anasema, shirika lilipata hasara ya Sh. 1.34 bilioni, kulinganishwa na faida ya Sh. 16.21 bilioni, iliyopata katika mwaka 2021/22.
Hata hivyo, CAG Kichere anaeleza, “…faida ya mwaka uliotangulia, haikutokana na biashara ambayo shirika imefanya. Faida ile, ilitokana na mauzo ya mali za shirika.”
Kutoana na hali hiyo, CAG Kichere amependekeza, shirika hilo kuongeza usanifu pamoja na kuishauri serikali kupitia upya mfumo wa utoaji wa ruzuku kwa mashirika ya umma ili kuhakikisha mfumo huo unazingatia tija na matokeo.
ZINAZOFANANA
Wanawake wasiojistiri vyema ni wachafu
Waumini wa Dini ya Kiislamu wapewa mwongozo
Sheikh Ponda: Mifumo ya uchaguzi irekebishwe