
John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika ameseme mbinu zinazotumiwa na msajili wa vyama vya siasa nchini ni kukitoa CHADEMA kwenye ajenda kuu ya Chama ya bila mabadiliko, hakuna uchaguzi, amtaka kueleza umma hatua zilizochukuliwa kwa uhaini unaofanywa na CCM. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).
Amesema hayo Leo tarehe 25 Machi 2025 wakati akifungua mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) na Baraza la vijana Chadema (BAVICHA) kutoka Kanda ya Kusini.
Amesema taarifa ya msajili wa vyama vya siasa ilimtaka katibu mkuu wa CHADEMA ndani ya wiki moja atoe majibu juu ya barua ambayo ameandikiwa inayohusu uhalali wa kikao cha baraza kuu la chama wa tarehe 22 Januari 2025 kilichothibitisha uteuzi wa katibu mkuu wa chama, naibu katibu mkuu na wajumbe wa kuteuliwa wa kamati kuu ya chama hicho.
Mnyika ameeleza kuwa, chama hicho kinaongozwa kwa mujibu wa katiba ambayo imeelezea uhalali wa vikao vya chama pamoja na akidi zake, amesema ibara ya 6. 22(a) ya Katiba ya chama inayohusu uhalali wa vikao vya chama.
Amefafanua kuwa ibara hiyo ina akidi za aina mbili za kikao, amesema kuna akidi ya vikao vya kawaida vya maamuzi ambayo inahitaji kuwepo na wajumbe asilimia 50, na kuna akidi ya vikao vya maamuzi maalumu kama kubadilisha katiba au uchaguzi, sera ya chama, vitahitaji akidi ya asilimia 75 ya wanachama.
Hivyo, kwa mujibu wa Mnyika; “kikao cha baraza kuu cha tarehe 22 Januari 2025, hakikuwa na ajenda ya uchaguzi bali kilikuwa na ajenda za kawaida, kwa sababu baada ya kuwa katibu mkuu nimepokea rufaa juu ya uchaguzi wa wajumbe wa kamati kuu wa kuchaguliwa, ajenda ya uchaguzi ikawa si sehemu ya kikao hicho.”
Aliendelea; “baada ya kuondoa ajenda ya uchaguzi kikao kikaendelea na ajenda za kawaida ambacho ni kuthibitisha uteuzi wa katibu mkuu na manaibu wake na wajumbe wa kamati kuu waliokuwa wamependekezwa na mwenyekiti.”
“Ajenda hizi za kawaida zinaongozwa kwa mujibu wa katiba ibara ya 6.22(A) kwamba akidi ya asilimia 50, katika kikao hicho idadi ya wajumbe wa Baraza Kuu waliokuwepo ambao walisaini wenyewe jumla yao ni 234 sawa na asilimia 56.8 na tunao ushahidi wa madhudhurio yao,” amesema Mnyika.
Amesema msajili wa vyama vya siasa ni mteule wa watawala kwa hiyo awaeleze watanzania hatua gani zimechukuliwa kwa CCM na viongozi wake kwa kuwa alikuwepo kwenye mkutano mkuu wa CCM wakati chama hicho kinakiuka katiba ya chama kwenye kumpitisha mwenyekiti wao kuwa mgombea pekee.
“Na msajili huyu ajitokeze aseme ni hatua gani amechukua kwa msemaji wa CCM kutoa tuhuma za uongo na za hatari, zenye kuvunja sheria na kuzua taharuki kwamba kampeni ya CHADEMA ya ‘Tonetone’ ya kukusanya michango, CCM imetoa madai kwamba CHADEMA inakwenda kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua virus vya Ebola na Mpox,” amesema Mnyika.
ZINAZOFANANA
Askofu Mwamalanga akemea vikali kauli ya Makala
Tundu Lissu atoa sababu za kutaka mabadiliko ya Uchaguzi
Slaa: Watanzania msidanganyike na propaganda za kitoto