
Askofu William Mwamalanga
ASKOFU William Mwamalanga na Mwenyekiti wa Kamati maalum ya Maaskofu na Masheikh, ambayo inashughulika na maswala ya Haki, Amani na Maadili kwa jamii amekemea vikali siasa ambazo zinachochea uvunjifu wa Amani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)
Akiwa kwenye mahojiano na kituo cha habari cha Jambo TV, leo 25 Machi 2025, amesema kufuatia taarifa inayosamba mtandaoni imezua taharuki na baadhi ya watu wamekuwa wakimpigia kuliza kama ni kweli viongozi wa siasa wanampango wa kuleta Ebola na Mpox.
Kwa mujibu wa Mwamalanga amesema kuwa taifa linaangaliwa kwa jicho la tatu hivo “kupitia hili wakome kabisa na huyo mtu, mwanasiasa ajiandae kwenda kijijini kwao, hata kimbilia kwenye chama chochote, hata CCM aondoke.”
Aliendelea “huwezi ukasema hayo, yaani ni kushindwa kuielewa nchi yako, siasa za namna hii haziwezi kuleta mabadiliko kwenye taifa, haziwezi kuleta ustawi wowote kwenye Taifa.”
Ameendelea kusema kuwa amekerwa sana na jambo hilo kwani kuna watoto wadogo wanaumwa huko mahospitalini hawajapata dawa madaktari wanawaza nini cha kufanya alafu kuna mtu mwingine anahamasisha vitu kama hivyo amesisitiza kuwa jambo hili lisionekane tena.
Amezitaka kamati za maadili kuchunguza hotuba za viongozi kabla hajazungumza kwa sababu zinapokuja taarifa kama hizi zinafanya watu mbalimbali wawe na hofu kubwa isiyokuwa na maana, ambayo inaweza kumdhuru hata aliyesema.
Mwamalanga amesema sasa ni wakati wa kuondokana na uongozi wa hila wa kuwadanganya watu, kwasababu siasa ya kweli ni kuwaonyesha watu kile ambacho chama kimefanyika kwenye uongozi wake na sio maneno yasiyo na tija.
Akizungumzia kauli mbiu ya CHADEMA ya ‘No Reform No Election’ Mwamalanga amesema tume imeanza vizuri kwa kuongeza siku za kujiandikisha…“Tusizuie uchaguzi tuwape nafasi tume, tufanye uchaguzi kwa sababu unaweza kwenda kupiga kura na kuhamasisha watu wapige kura, wawe wengi, alafu kama kuna kitu chochote kitakuwa kinyume na haya matazamio tunayoyataka tutakubaliana na CHADEMA kwamba kweli ‘No Election’ maana kwenye ‘Reform’ kumeonyesha mashaka”.
Aliendelea..”kwahiyo ni kama sasa CHADEMA wamemfichua mtanzania, wamemfunua kwamba mahali unapoona kuna tatizo au uchaguzi una kwenda kusukumizwa na polisi. Polisi hatutaki awe msimamizi wa uchaguzi, tumekuwa na chaguzi huko nyuma wasimamizi polisi kazi yao wakaicha kule wakaenda kusimamia uchaguzi, tunataka Tume yenyewe isimamie uchaguzi, isikilize na kukubaliana na wananchi Mahali ambapo kuna tatizo.
ZINAZOFANANA
Hatua za msajili analenga kuinyamazisha ajenda ya Chadema
Tundu Lissu atoa sababu za kutaka mabadiliko ya Uchaguzi
Slaa: Watanzania msidanganyike na propaganda za kitoto