
Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, Amani Golugwa
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Amani Golugwa, amesema chake, kitaanza mikutano ya hadhara nchi nzima, kuanzia 23 Machi mwaka huu. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 19 Machi 2025, Golugwa amesema, kwa mujibu wa ratiba ilivopangwa, mikutano hiyo itaanzia rasmi katika Kanda ya Nyasa na mkutano wa kwanza utafanyika jijini Mbeya.
Amesema, lengo la mikutano hiyo, inayofanywa na Chadema nchi nzima, ni kuwaelimisha wananchi juu ya alichokiita, “No Reforms, No Election” – Hakuna Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi.
Kwa mujibu wa Golungwa, mikutano hiyo, itahudhuriwa na viongozi wakuu wote wa Chadema, wakiwamo wenyeviti wa mabaraza ya chama hicho.
“Mikutano yetu itahudhuriwa na viongozi wote wakuu, wakiwamo wenyeviti wa Bazecha (Baraza la Wazee), Bavicha (Baraza la Vijana) na Bawacha (Baraza la Wanawala); wajumbe wa Kamati Kuu (CC) na Sekretarieti,” alifafanua.
Aliongeza, “Tunataka kutumia mikutano hiyo, kuwafafanulia wananchi kile ambacho sisi tunakiamini kwa kipindi hiki. Kwamba, taifa linahitaji mabadiliko.
“Kwa hiyo, tuondoke kwenye swaga. Sasa hivi, ni No Reforms, No Election. Huu ndio wimbo unaostahili kufikishwa kila mahali. Tunapaswa kuhakikisha unaimbwa mtaani na vijiweni.”
Akizungumza kwa kujiamini, Gologwa amesema, “tuanze kuyazungumza hayo. Tueleze ni mabadiliko gani ambayo tunayataka.”
Aidha, Golugwa amesema, viongozi wa chama hicho watawaeleza wananchi ya mabadiliko yanayotakiwa, kuanzia kwenye Katiba, hadi kwenye muundo wa Tume ya uchaguzi na utendaji wake.
“Tutazungumza kuhusu muundo wa majimbo. Tutaeleza kuwa Katiba ya nchi iondoke kwenye kile kinachosemwa kwamba majimbo yatagawanywa kwa kuangalia hali ya kijipgrafia na miundombinu,” amefafanua.
Amesema, “Katiba iwekwe wazi kuwa universal standard kwamba wananchi ndio wanao wakilishwa kwenye Bunge sio hali ya jiografia na miundombinu.
Amesema, “Kwa hiyo, mgawanyo wa majimbo, utokane na idadi ya watu; kila kura ya mwananchi iwe na thamani kwenye majimbo yote. Haya ndio mabadiliko tunayopaswa kuyazungumza.”
Kwa mujibu wa Golugwa amesema, wananchi wataelimishwa juu ya matatizo ambayo wamepitia wagombea wa vyama vya upinzani kuenguliwa pamoja na dosari za uchaguzi ambazo zinatokea huku mamlaka zikifumbia suala hilo macho.
Amesema, “…ninyi wanahabari mnaripori karatasi feki za kura. Zile karatasi feki za kura hakuna mtu wa upinzani anaweza kuzichapisha.
“Karatasi feki za kura zinakutwa vituoni halafu anasimama mtu mwenye dhamana anatuambia watu wote 60 milioni, kwamba uchaguzi uko sawa, umeenda vizuri. Haya ni matusi.
“Ni kama unaona Watanzania wote hawaoni hizi dosari…dosari hizi zote lazima tuzungumze kwamba tunahitaji mabadiliko haya.”
Kwa mujibu wa Golugwa, katika awamu hii ya kwanza ya mikutano, Chadema kimekusudia kuelimisha wananchi na juu ya kauli mbiu ya bila mabadiliko hakuna uchaguzi.
Amesema, kabla ya uchaguzi kufanyika, ni sharti kufanyike mabadiliko ya msingi.
Chadema hakina dhumuni la kukimbia wala kususia uchaguzi.
ZINAZOFANANA
Wassira amchongea Mo Dewji kwa serikali kwa kutelekeza mashamba ya Rungwe
OMO afunguka mazito waliyokutana nayo Angola
Watanzania watakiwa kuipiga chini CCM