March 13, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

ACT yabadili mwelekeo wa kufanya siasa

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman

 

MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud amesema chama hicho kimeamua kubadili mwelekeo wa kufanya siasa hapa nchini kutoka katika siasa za maridhiano kwasababu siasa zinazohitajika kwa wakati huu ni siasa za mapambano. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).

Haya ameyazungumza leo 12 Machi 2025 wakati wa uzinduzi wa kongamano la viongozi wa chama hicho mkoa wa Dar es salaam, akieleza kuwa tulipotoka tuliaminishwa tunaenda kwenye siasa za maridhiano lakini mwelekeo ulivo sasa si kama ilivoahidiwa.

Amesema Chama hicho kilihakikisha kinashirikisha viongozi wastaafu wa Chama cha mapinduzi katika ngazi zote juu ya suala la maridhiano kwa sababu ya kuamini katika siasa za kistaarabu, ambazo zitawapa waTanzania fursa ya kutengeneza nchi yao lakini malipo ilikuwa ni pamoja na viongozi wa chama hicho kutekwa na kuteswa.

Othman amesema pamoja na hayo chama kilipigania kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi na kwa mujibu sheria ilipitisha kufanyika mabadiliko katika tume hiyo ambayo haijabadilishwa chochote zaidi ya kulaghai watu kama watoto wadogo, amesisitiza.

“Tume yetu imekuwa kama muigizaji Joti, akivaa nguo za kike anaitwa Kiboga, akivaa nguo za shule anaitwa Andunje. Na sisi Tume yetu kila kitu kile kile eti wanataka tuamini ni Tume huru ya Uchaguzi hii ni kiboga kavaa kaptula.”

Ameeleza namna ambavyo uchaguzi wa serikali za mitaa ulivyoidhihirisha tabia ya Chama cha Mapinduzi katika kuendesha nchi pamoja na kuwakatisha tamaa watanzania na wale waliokuwa na matumaini na Tanzania kuwa inaanza kusonga mbele , nchi ambayo wananchi wake ni maskini lakini wamekaa juu ya utajiri uliopindukia.

Aidha Othman ameeleza kuwa, baada ya yaliyotokea kwenye serikali za mitaa wapo baadhi ya watu upande wa vyama vya upinzani na ndani ya chama walidhani kuwa chama hakifanyi siasa zinazostahili yaani siasa za mapambano, amesisitiza kuwa badala ya kutafta adui tunatafta mchawi ndani yetu wenyewe.

Othman amesema maoni ya watu yamekuwa mengi juu ya suala la siasa hapa nchini kwa sababu ilipoanza awamu ya sita matarajio yalikuwa kuliponya taifa na kuwapa matumaini watanzania kutokana na kuathiriwa na siasa na matokea ya chaguzi za mwaka 2015/2020, baadae mwenyekiti wa chama hicho alipokuja kwenye mkutano mkuu wa ACT alisema kwamba kama uchaguzi wa 2020 ungesimamiwa ipasavyo kwa sheria kusingekuwa na matatizo, na akasisitiza katika mkutano huo chaguzi zinazokuja zitakuwa huru na za haki lakii haijawa hivo.

Vilevile amesema chama cha ACT Wazalendo kimeshiriki kikamilifu kusimamia 4R za Rais Samia ili kupata haki pamoja na hayo chama kimefungua kesi nyingi mahakamani ili kupata tafsiri za sheria mahakamani, yaani chama kilifanya siasa kwa mujibu wa hali ilivyokuwa ili kuwepo na maridhiano ya haki lakini sasa Chama kimeadhimia kushirikina na vyama vyenye nguvu na utayari ili kupambania demokrasia ya nchi yetu.

About The Author

error: Content is protected !!