March 10, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wanachama wa NHIF waruhusiwa kutumia NIDA kupata huduma

Mkurugenzi NHIF, Irene Isaka

 

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk. Irene Isaka amesema kwa sasa mwanachama wa mfuko wa NHIF halazimiki kuwa na kadi ya bima, kwani kwa sasa hata namba ya kitambulisho cha Taifa inaweza kutumika kupata huduma. Anaripoti Apaikunda Mosha. Dodoma…(endelea).

Amezungumza na waandishi wa habari leo 10 Machi 2025, kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mfuko huo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

Amesema bima hii inawafikia 8% ya watanzania mpaka sasa, pia kumekuwa na ongezeko la vituo ambayo mpaka sasa vipo 14,000 ikiwa sehemu kubwa ya vituo hivo ni vya serikali na vingine vya watu binafsi.

Ameeleza kwamba TEHAMA imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza muda wa uchakataji wa taarifa pamoja na matumizi ya makaratasi na badala yake kutumia mfumo wa e-office ambao umerahisisha shughuli nyingi za uchakataji wa taarifa wa taarifa zote.

Pia mfumo huu umewezesha wanachama kujisajili wenyewe, kupunguza muda wa kuchakata madai na kuondoa viashiria vyote vya udanganyifu na malipo ya michango kwa mfumo wa kieletroniki.

“Kupitia mfumo huu NHIF imeweza kusajili wanachama 2,200,000 kati yao wanachama 2,840,543 wamesajiliwa katika kipindi cha miezi sita, aidha ukusanyaji wa michango  umeongezeka hadi kufikia Sh. 2.3 trilioni na kati ya hizo asilimia 92 ni michango ya wanachama huku asilimia 7 ikiwa pato uwekezaji na asilimia 1kutokana na juhudi za serikali,” amesema Dk. Irene.

Aidha, ameeleza kuwa mfuko umeweza pia kuokoa zaidi ya Sh. 22 bilioni kwa kupungua hali ya udanganyifu, kati ya chunguzi zilizofanyika kwenye vituo 259  zaidi ya kadi 13,000 za wanachama zimefungiwa, vituo 11 vimefungiwa pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria watumishi ambao wamehusika na udanganyifu kwa namna yoyote. 

Dk. Irene amesema kuwa  lengo la NHIF ni kuongeza wigo kwa wanachama aidha, ikishirikiana na tamisemi wanaweza kutambua kaya zenye uhitaji maalumu ili waweze kupata bima ya afya na kupitia sekta binafsi, madalali na mawakala wa bima wanaweza kufikia jamii nzima.

About The Author

error: Content is protected !!