
SERIKALI ya Tanzania, imepanga kuanza kununua umeme kutoka Ethiopia, ili kukabiliana na uhaba wa nishati hiyo, katika mikoa ya kanda ya Kaskazini. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).
Rais wa Jamhuri, Samia Suluhu Hassan ameliambia taifa jana Jumapili, kwamba serikali yake, imeanza kukamilisha mchakato wa kununua umeme nje maalumu kwa ajili ya mikoa hiyo ya kaskazini mwa Tanzania.
“Serikali yenu inachukua hatua ya kununua umeme nje maalum kwa mikoa ya kaskazini ili umeme upatikane masaa 24 bila kukatika, tupo katika hatua za mwisho kusaini mikataba ili kununua umeme ule uungwe kanda ya kaskazini” alisema rais Samia hatika hotuba yake.
Samia ameyasema hayo wakati akizindua mradi wa maji wa Same- Mwanga- Korogwe.
Haya yanajiri wakati Tanzania imekamilisha kwa zaidi ya asilimia 90, ujenzi wa bwawa la kisasa la kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), lililopo Rufiji mkoani Pwani.
Bwawa la Nyerere litaweza kuingiza kwenye gridi ya taifa, megawati 2115 za umeme na kwamba umbali kutoka Ethiopia hadi Moshi, mkoani Kilimanjaro, ni kilomita 2011.
Lakini umbali wa kutoka Chalinze, mkoani Pwani ambako kumejengwa mtambo wa kupokelea umeme unaozalishwa Rufiji, hadi Moshi, ni kilomita 471.
Mradi wa ujenzi wa umeme wa bwawa la Nyerere, unajengwa na kampuni ya Arab Contractors na Elsewedy Electric, kutoka Misri, unatarajiwa kutumia zaidi ya Sh. 7.8 trilioni, hadi utakapokamilika.
ZINAZOFANANA
Mramba afafanua mradi wa umeme kutoka Ethiopia
Asilimia 22 ya vijana wanakumbwa na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa
TMA yatangaza uwepo wa Kimbunga ‘JUDE’ rasi ya Msumbiji