
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imeuahairisha mchezo wa Yanga dhidi ya Simba uliokuwa uchezwe leo saa 1:15 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na sintofahamu iliyotokea jana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kamati hiyo imeahairisha mchezo wa huo ili kutoa nafasi ya kupata taarifa zaidi zitakazosaidia kutenda haki mara baada ya Simba kugomea mchezo.
Katika taarifa yao Bodi ya Ligi imeeleza kuwa, mapema kabisa ilipokea barua kutoka kwa klabu ya Simba kuhusu kuzuiliwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kinyume na kanuni.
Baada ya kupokea barua hiyo, bodi ya Ligi iliwaagiza maafisa wake wote wanahusika kwenye mchezo huo, ambao walishuhudia tukio hilo kutuma ripoti ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.
Maamuzi hayo ya bodi ya ligi kuahirisha mchezo huo, yamefanyika kupitia kikao chake cha dharura kilichokaa leo tarehe 8 Machi 2025.
ZINAZOFANANA
Kadinali Robert Prevost atangazwa kuwa Papa mpya
Bunge la Ulaya laitaka Tanzania kumuachia huru Lissu
G55 watimka Chadema