
Rose Mushi, Mwenyekiti wa Bawacha Kanda ya Pwani
MWENYEKITI wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Kanda ya Pwani, Rose Mushi, amesema kuwa baraza la wanawake wa chama hicho wataadhimisha Siku ya Wanawake Duniani tarehe 8 Machi 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Apaikunda Mosha. Dar es Salaam … (endelea).
Amezungumza hayo leo tarehe 26 Februari 2025, Rose amesema mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu aidha maadhimisho hayo yata hudhuriwa na viongozi wa chama na wanachama.
Katika siku ya maadhimisho hayo, Rose amesema, viongozi na wanachama watakuwa na wasaa mzuri wa kuelimishana maswala ya kisiasa, ujasiriamali pamoja na kutiana moyo na ujasiri dhidi ya maridhiano ya Chama hicho kwamba ‘Hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi’.
Rose ametoa ufafanuzi juu ya shughuli ambazo zitafanywa na wanachama kuelekea siku hiyo amesema, BAWACHA wakishirikiana na viongozi wa kitaifa watafanya shughuli za kijamii, siku ya tarehe 1 Machi hadi 7 Machi, ndani ya mikoa mitano na majimbo 19 ya kanda ya Pwani, kuelekea kilele cha siku hiyo ya wanawake duniani
“Wanachama watatembelea vituo vya watoto yatima, watakwenda kutoa misaada kwenye vituo vya kulea wazee, wataenda mahospitalini kuwafariji wagonjwa, kufanya usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti,” amesema Rose.
Aidha akizungumza kwa niaba ya BAWACHA mkoa wa Pwani Rose amesema Kanda ya Pwani wanakaribisha wanawake wote wanachama na wasio wanachama kutoka sehemu mbalimbali kuhudhuria kwa wingi katika madadhimisho hayo.
ZINAZOFANANA
Aliyemuua mkewe na kumchoma moto ahukumiwa kunyongwa
JKCI kinara utoaji huduma ya afya Afrka Mashariki na Kati
Rais Samia aweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara na daraja Pangani