
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imejinadi kuwa ni kati ya hospiatli mahili barani Afrika,inayofanya matibabu ya ubadilishadi wa valvu ya moyo bila kufungua kifua. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)
Hayo yameelezwa na Dk. Peter Kisenge Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa maendeleo ya utekelezaji wa hospitali hiyo kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Habari Maelezo.
Mkurugenzo huyo amesema katika kuboresha huduma za afya mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni uliogharimu shilingi milioni 526,604,116 umefungwa katika Hospitali ya Dar Group.
Ameeleza kuwa mtambo mwingine wa kuzalisha hewa ya oksigeni wenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 umefungwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Dk. Kisenge amesema kuwa taasisi hiyo ni hospitali maalum na Chuo Kikuu cha mafunzo ya utaalamu wa matibabu ya moyo inayomilikiwa na Serikali inayotoa mafunzo na huduma za utafiti wa moyo.
Amesema kuwa Kwa kipindi cha miaka minne hospitali hiyo imeona jumla ya wagonjwa 745,837 kati ya hao watu wazima walikuwa 674,653 na watoto 71,184 wagonjwa waliolazwa walikuwa 30,645 watu wazima wakiwa 25,273 na watoto 5,372.
Amesema kuwa wagonjwa waliotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Upanga walikuwa 513,484 kati ya hao watu wazima 470,119 na watoto 43,365 wagonjwa waliolazwa walikuwa 17,668 watu wazima wakiwa 14,580 na watoto 3,088.
Mkurugenzi huyo pia amezungumzia huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kuwa ni pamoja na matibabu ya moyo, kinywa na meno, huduma za dharura, kliniki ya wanawake na wajawazito, kliniki ya watoto, macho, pua, masikio na koo, kliniki ya ngozi, vibofu vya mkojo, upasuaji mkubwa na mdogo, magonjwa ya tumbo na ini, figo na matibabu mengine ya magonjwa yanayoambukiza kama malaria.
Kuhusu huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Dk. Samia Suluhu Hassan Outreach Services amesema kuwa zimetolewa katika mikoa 20 na maeneo ya kazi 14 kwa watu 21,324 watu wazima wakiwa 20,112 na watoto 1,212 walifanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo.
Amesema kuwa kati ya hao 8,873 watu wazima wakiwa 8,380 na watoto 493 walikutwa na matatizo mbalimbali ya moyo na kuanzishiwa matibabu.
“Wagonjwa 3,249 watu wazima 2,765 na watoto 484 walikutwa na matatizo yaliyohitaji matibabu ya kibingwa na kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.
“Wataaamu wetu walivuka mipaka ya nchi na kwenda kutoa huduma za matibabu ya moyo katika nchi za Malawi, Zambia na Jamhuri ya Watu wa Comoro wakiwa katika nchi hizo walitibu wagonjwa 1,189 watu wazima walikuwa 851 na watoto 338. Wagonjwa 262 walipewa rufaa ya kuja kutibiwa JKCI,” ameeleza Mkurugenzi Kisenge.
Katika hatua nyingine amesema.kuwa wagonjwa waliotibiwa kutoka nje ya nchi walikuwa 689.
“Wagonjwa hao walitoka katika nchi za Somalia, Malawi, Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Watu wa Comoro , Msumbiji, Nigeria, Siera Leone, Zimbabwe, Zambia, Uganda, Congo, Ethiopia, Burundi na wengine kutoka nje ya Afrika zikiwemo nchi za Armenia, China, Ujerumani, India, Norway, Ufaransa na Uingereza.
“Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua na kubadilishwa Valvu za moyo moja hadi tatu, upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu ya moyo (Coronary Artery Bypass Graft Surgery –CABG), upasuaji wa mishipa ya damu na mapafu walikuwa 2,784 kati ya hao watu wazima walikuwa 1,880 na watoto 904.”amesema.
Mwisho.
Aidha amesema kuwa Shilingi bilioni 2.16 zilitolewa na Serikali kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya watoto mahututi na chumba cha wagonjwa mahututi cha watu wazima, ukarabati na utanuzi wa ICU ya watoto ambayo hapo awali ilikuwa na vitanda nane na hivi sasa inavitanda 16 na ICU ya wakubwa ambayo imetanuliwa na kuwa na vitanda kumi kutoka nane ambapo shilingi 503,450,051 zilitumika katika ukarabati huo.
Ameeleza kuwa Shilingi 1,465,683,469 zilitumika kununua vifaa tiba, shilingi 170,000,000 zilitumika kwa ajili ya tiba mtandao (Telemedicine) na shilingi 28,340,000 zilitumika kugharamia mafunzo ya wataalamu wa fani ya radiolojia na huduma za wagonjwa mahututi.
Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeajiri wafanyakazi wapya 186 wa kada mbalimbali, wafanyakazi 366 wamepandishwa vyeo katika madaraja mbalimbali. Taasisi iliwaongezea ujuzi wa kazi wafanyakazi kwa kuwapeleka kozi na muda mfupi watumishi 184, waliomaliza masomo ya kozi za muda mrefu ni 45 na waliopo masomoni ni 51.
ZINAZOFANANA
Lissu mgeni rasmi Siku ya Wanawake Duniani Mlimani City
Aliyemuua mkewe na kumchoma moto ahukumiwa kunyongwa
Rais Samia aweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara na daraja Pangani