
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuashiria ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Bagamoyo (Makurunge)-Pangani -Tanga lenye kilomita 256 pamoja na Daraja la mto Pangani urefu wa mita 525. Anaripoti Apaikunda Mosha. Tanga … (endelea).
Akizungumza na wakazi wa Pangani mkoani Tanga tarehe 26 Februari 2025. Rais amesema kazi hiyo imefanyika kwa lengo la kubadilisha uchumi wa Pangani, pamoja na dhamira ya kuiunganisha Tanga na baadhi ya mikoa/ushoroba au kanda za kiuchumi.
Aidha Rais Samia amesema eneo hilo la Bagamoyo Serikali inatarajia kujenga Kongano (EPZ) la viwanda ili kukuza uchumi, pamoja na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo itakayounganisha Tanga kupitia Pangani, Bandari ya Mombasa na Bagamoyo kwenye uhuru wa uchumi.
Pia amesema kuwa Serikali imepanga kukuza uchumi wa buluu kwa kuboresha upatikanaji wa masoko ya bidhaa za baharini ili kuongeza fursa za ajira kwa wakazi wa eneo husika.
Rais ameainisha miradi mingine ambayo inatarajiwa kuanzishwa Pangani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha sukari pamoja na soko la kimataifa la samaki ivo amewataka wanatanga kutumia fursa hizo kukuza uchumi wa nchi.
Pamoja na hayo Samia Suluhu Hassan ametoa boti kubwa za kisasa 120 pamoja na boti saidizi 118 kwa nchi nzima na kwa upande wa mkoa wa Tanga, amekabidhi boti kubwa 30 kati ya 35 pamoja na boti saidizi 60 zenye uwezo wa kubeba tani tatu mpaka tano za samaki kwa lengo la kuwawezesha wavuvi kufanya kazi zao vizuri.
ZINAZOFANANA
Lissu mgeni rasmi Siku ya Wanawake Duniani Mlimani City
Aliyemuua mkewe na kumchoma moto ahukumiwa kunyongwa
JKCI kinara utoaji huduma ya afya Afrka Mashariki na Kati