
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema kiasi cha Sh. 12 bilioni zimetengwa kwenye Mradi wa HEET kwa ajili ya ujenzi wa Kampasi ya Chuo kikuu cha Mzumbe mkoani hapo. Anaripoti Apaikunda Mosha, Tanga … (endelea).
Akizungumza baada ya ufunguzi rasmi wa Shule ya Sekondari ya Sayansi ya Wasichana ya Kilindi leo Jumanne 25 Februari 2025, Mkenda amesema Tanga ni miongoni mwa mikoa ambayo Rais alisema kujengwe Kampasi ya vyuo vikuu, hivyo Chuo hicho kitajengwa ukingoni mwa mji huo wilaya ya Mkinga.
Aidha Mkenda amesema mkoa wa Tanga umeendelea kuwa kinara katika kutekeleza magizo ya Rais Samia ya ujenzi wa shule za sekondari ili kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa huduma za elimu katika kila mkoa.
Ameongeza kwa kusema kuwa, kufuatia agizo la Rais la ujenzi wa shule, kwa sasa shule sita za sekondari za mafunzo ya amali zinajengwa mkoani Tanga, hasa katika maeneo yasiyo na vyuo vya VETA, ili kuongeza ujuzi wa ufundi kwa vijana, amesema ujenzi huo umekamilika katika maeneo mengi, isipokuwa Handeni na Muheza ambapo kazi bado inaendelea.
Aidha Mkenda amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo ya Sayansi ya wasichana katika mkoa wa Tanga ni sehemu ya mpango mkubwa wa mageuzi katika sekta ya elimu, unaolenga kuboresha upatikanaji wa elimu ya sayansi kwa wasichana.
ZINAZOFANANA
Rais Samia azindua shule ya sekondari ya wasichana Kilindi
Vodacom Foundation kufadhili kongamano la Utafiti wa Elimu Tanzania 2025
Sekretarieti ya Ajira yatoa ufafanuzi ajira za walimu