November 23, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

TPA yawavutia wengi maonesho nanenane Dodoma

 

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema inayachukulia maonesho ya wakulima maarufu kama ‘Nane nane’ kwa uzito wa kipekee kwani mbali ya kutoa fursa kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na watanzania kujua maendeleo ya sekta ya bandari pia kuzitangaza huduma zitolewazo na mamlaka hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na wageni mbalimbali waliofika kwenye Banda la Bandari ndani ya viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma ambako maonesho ya Nanenane yanaendelea kitaifa, Meneja Mahusiano wa Mawasiliano wa TPA, Nicodemus Mushi amesema watu wengi wamejitokeza kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali za bandari.

“Kuna mageuzi makubwa sana yamefanyika katika sekta ya bandari hapa nchini kwani miradi mingi mikubwa imetekelezwa na mingine ipo katika utekelezwaji wa hatua mbalimbali,” amesema na kuongeza kuwa nanenane inawapa wadau, wateja na umma nafasi ya kujifunza furs ana huduma zinazotolewa.

Mushi alisema kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo cha Bandari ni fursa ya ajira kwa vijana kwani ndiyo wanatumiwa au kuajiriwa kwenye bandari za Bahari na zile zilizopo kwenye maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

“Bandari imekuwa ni kiungo muhimu sana wakulima kwani bandari zetu zinatumika kusafirisha mazao kwenye masoko ya kimataifa,” alisema meneja uhusiano na mawasiliano huyo.

Aliwahimiza watanzania kuchangamkia fursa na huduma zinazotolewa na TPA pamoja na vituo vyake vilivyopo kwenye nchi mbalimbali zikiwemo Jamhuri ya Kongo, Rwanda, Zambia, Burudi, Uganda na Zimbabwe.

Kwa upande, Mkurugezi wa Kampuni inayoingiza mbolea ya Premium Agro-Chem, Kamlesh Asawla kampuni yake ni mtumiaji mkubwa bandari kati kuingiza na kusafirisha mizigo kutoka nje ya nchi.

“Tumeshaingiza shehena ya mbolea tani elfu kumi (10,000) inasubiri kupakuliwa. Tumekuwa wateja bandarini tangu mwaka 1994 kampuni yetu ilipoanzishwa,” alisema Bw Asawla alisema na kuwataka watanzania wengi kujitokeza kwenye maonesho ya Nanenane Dodoma.

Alisema kufuatia umuhimu wa maonesho hayo, Kampuni ya Premium Agro-Chem inashiriki katika maonesho ilikukutana na wakulima na wakulima na mawakala wa mbolea.

About The Author