February 23, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mbowe afungua Mkutano Mkuu akilia na matusi

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

 

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amewasihi viongozi watakaoshika nyadhifa katika chama hicho ni lazima wakijenge katika misingi ya maadili na nidhamu. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Haya ameyasema leo tarehe 21 Januari 2025 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa chama hicho, unaoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Mtakaopewa mikoba ya chama hiki, lazima mkarekebishe mambo, inawezekana tukavumilia matusi kipindi hiki cha uchaguzi lakini msingi wa Chadema sio matusi watakaokabidhiwa mikoba leo wakasafishe,” alisema Mbowe.

Hiki chama tunawajibu wote kukilinda kwa gharama yoyote ile na chama hichi tutakilinda.

Mbowe amesema kuwa Chadema kitamaliza uchaguzi wakiwa wa moja na kwamba uchaguzi huo sio vita.

“Uchaguzi huu haupaswi kuwa vita unapaswa kuwa ujenzi ya Demokrasia. Wapo watabiri wengi walisema kuhusu Chadema , Mheshimiwa Mbowe mnakwenda kukipasua Chadema,” amesema Mbowe.

Amesema kuwa Chadema kimebeba ndoto ya Taifa, sio ndoto ya kiongozi mmoja mmoja, tutaendelea kupita katika mabonde na milima lakini kila mmoja wetu awe na wajibu wa kukilinda Chadema na njia ya kukilinda ni kuwa hekima na nidhama.

“Kazi tunatowaachia warithi wa chama hichi ni kujenga misingi ya maadili na nidhamu, matusi sio msingi wa Chadema,” amesema Mbowe

About The Author

error: Content is protected !!